Back to top

Sabbath Bible Lessons

Masomo katika Waraka wa Yakobo

 <<    >> 

Utangulizi

Waraka wa Yakobo ni moja kwa moja. Jinsi tunavyohitaji jumbe ndani yake hivi sasa! Hivyo kwa muda wa miezi mitatu ijayo, wanafunzi wa shule ya shule ya sabato Ulimwenguni kote watakuwa wakijishughulisha na Masomo katika Waraka wa Yakobo. Mambo muhimu juu ya ushawishi wa ulimi (kwa mema au mabaya) utii kwa mungu kwa imani, nguvu ya maombi, na mfano wa Eliya ni wa haki. Mada chache muhimu. Kwa nini haya yote yanafaa sana leo?

“Dhambi ya zama hizi ni kupuuza amri za Mungu zilizo wazi. Nguvu ya mvuto kuelekea uelekeo potofu ni kubwa sana.”—Testimonies for the Church, vol. 3, p. 483.

“Hebu wasiwepo watu wanaojidanganya kwa kuamini kwamba wanaweza kuwa watakatifu wakati wanavunja mojawapo ya matakwa ya Mungu kwa makusudi. Kuendekeza kutenda dhambi inayojulikana kunanyamazisha sauti ya Roho anayetushuhudia na kumtenga mtu mbali na Mungu. “Dhambi ni uvunjaji wa sheria.” Na “kila atendaye dhambi [avunjaye sheria] hakumwona yeye wala hakumtambua.” 1 Yohana 3:6. ”—The Great Controversy, p. 472.

“Leo panahitajika sauti ya kukemea vikali; kwa maana dhambi kuu zimewatenganisha watu wa mungu. Kukosa uaminifu kumekuwa kama mtindo wa maisha. ‘hatumtaki huyu atutawale,’ ndiyo lugha ya maelfu ya watu. Luka 19:14. mahubiri laini yanoyohibiriwa mara nyingi hayaleti mguso wa kudumu; tarumbeta haitoi sauti fulani. Wanadamu haguswi mioyoni na ukweli ulio wazi wenye makali wa Neno la Mungu.

“Kuna watu wengi wanaodai kuwa Wakristo, ikiwa wangeonyesha hisia zao za kweli, wangesema, kuna haja gani ya kusema waziwazi hivyo? Wanaweza pia kuuliza, kwa nini Yohana Mbatizaji alilazimika kuwaambia Mafarisayo, ‘Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliwaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?’ Luka 3:7. kwanini aliikemea hasira ya Herode kwa kumwambia Herode kwamba ilikuwa ni kinyume cha sheria kwake kuishi na mke wa ndugu yake? Mtangulizi wa Kristo alipoteza maisha yake kwa uwazi wake akizungumza. Kwa nini hangeweza kusonga mbele bila kutokubarika kwa wale waliokuwa wakiishi katika dhambi?

“Kwa hiyo watu wanaopaswa kusimama kama walinzi waaminifu wa sheria ya mungu wamebishana, mpaka sela imechukua nafasi ya uaminifu, na dhambi inaendelea bila kukemewa. Ni lini sauti ya karipio la uaminifu litasikika tena kanisani?”—Prophets and Kings, pp. 140, 141.

“Utoshelevu umewekwa kwa kila kwa kila mwana na binti ya Adamu kupata kujuakwa ubinafsi mapenzi ya Mungu, kuikamilisha tabia ya Kikirsto na kutakaswa kupitia ukweli.”—Testimonies for the Church, vol. 2, p. 644.

Kwa kweli tunahitaji msaada wa mungu na tunahakikishiwa waziwazi kwamba “ Kwa kila maombi ya dhati yanayowekwa kwa imani kwa lolote, majibu yatarudishwa. Huenda yasije kama tulivyotarajia; lakini yatakuja, si labda kama tulivyopanga, lakini wakati ule tunapoyahitaji sana.”—Ibid., vol. 3, p. 209. Amen!

Idara ya shule ya sabato GC

 <<    >>