Back to top

Sabbath Bible Lessons

Masomo katika Waraka wa Yakobo

 <<    >> 
  SABATO, NOVEMBA 2, 2024

Sadaka za sabato ya kwanza kwa ajili ya mkutano mkuu Idara ya Fasihi

Kuna msemo maarufu, tone la wino linaweza kutengeneza fikara milioni.” Nyenzo zilizochapishwa huelekea kubeba uzito zaidi kuliko tu maneno yanayosemwa kwa kiasi kikubwa kutokana kudumu kwake. Kwa maandishi, tunaweza kuchua muda wa kusoma kwa kasi yetu wenyewe, na pia kurejelea nyuma na kufikiria kwa undani zaidi habari tunayotafuta kujifunza. Inasaidia wakati wa kujaribu kuchukua mada za kina za kiroho.

Hili limekuwa kweli katika historia: “Kalamu ya Luther ilikuwa na nguvu, na maandishi yake, yaliyotawanyika, yalisisimua ulimwengu. Mashirika hayo hayo yapo chini ya amri yetu, na vifaa vimeongezeka mara mia. Biblia, machapisho katika lugha nyingi, yanayoeleza kweli kwa wakati huu, yako karibu nasi na yanaweza kubebwa upesi hadi ulimwenguni kote. ”—Testimonies for the Church, vol. 6, p. 403.

“Na kwa kiwango kikubwa kupitia nyumba zetu za uchapishaji inapaswa kutimizwa kazi ya yule malaika mwingine anayeshuka kutoka mbinguni kwa nguvu kubwa na ambaye huangaza dunia kwa utukufu wake. ”—Ibid., vol. 7, p. 140.

Mnamo 1849, James White alitoa kichapisho kidogo kiitwacho Ukweli wa sasa. Mafungu madogo ya Makala yaliwekwa chini sakafuni. Ndipo ndugu na dada wakayazunguka na kumsihi Mungu kwa machozi kuzibariki nakala hizi zinapotumwa. Nakala hizo zilikusanywa zikafungwa na kutumwa, naye James White akazipeleka. Maili nane hadi kwenye ofisi ya posta ya Middletown.”—Early Writings, (xxv).

Kitendo hiki kilikuwa ni kujibu ujumbe huu: “unapaswa kuanza vijizuu na kuwatumia watu. Mwanzoni viwe vichache; Lakini kadri watu wanavyosoma, watakutumia fedha za kuchapishia, na itafaulu tangu mwanzo.’ ”—Ibid., (xxiv).

Nini hufanyika wakati gharama za usafirishaji zinapoongezeka na vizuizi vya mipakani vikihitaji njia za ghalama kubwa zaidi za usambazaji? Bei yetu ya usajiri haitoi gharama hizi mpya. Kwa hiyo, ni lazima tutegemee ukarimu wenye fadhili wa waumini wenzetu ili kutimiza unabii ulioambiwa kwa mhubiri huyo wa awali:

“Kama watu wanavyosoma, ndivyo watakavyokutumia. ”

Tunaomba sadaka hii ya sabato ya kwanza kwa idara ya Fasihi ya GC itagusa moyo wako ili kutoa ziada kwa ajili ya roho duniani kote zinazohitaji kusoma ukweli wa sasa. Asante!

Ndugu zenu katika Idara ya Fasihi ya Mkutano Mkuu

 <<    >>