Jumapili
Novemba 10
1. KUTULIZA NAMNA YETU
a. Ni nini chapasa kuwekwa akilini na wale ambao siku zote ni wepesi kujaribu kuwatawala wengine? Yakobo 3:1; Marko 9:35.
“Mungu anamwajibisha kila mtu kwa ushawishi unaozunguka nafsi yake, kwa sababu yake mwenyewe na kwa ajili ya wengine. ”—Counsels to Parents, Teachers, and Students, p. 102.
“Kwa kawaida, wanadamu wana ubinafsi na maoni yao. Lakini ubinafsi hutoweka katika maisha ya wale wanaojifunza masomo ambayo kristo anatamani kuwafundisha. Wanakuwa washirika wa asili ya Kimungu, na kristo anaishi ndani yao. Wanawachukulia watu wote kama ndugu, wenye matarajio sawa, uwezo, majaribu, wakitamani huruma na wanaohitaji msaada.
“Kamwe hatupaswi kumdhalilisha kiumbe mwenzetu. Tunapoona kwamba makosa yamefanywa tunapaswa kufanya yote tuwezayo kuwasaidia wale ambao wamekosea, kwa kuwaambia uzoefu wetu wenyewe tulifanya makosa makubwa sana, subira na ushirika, fadhili na usaidizi, kwa upande wa wafanyakazi wenzetu, vilitupa ujasiri na tumaini.“ —The Signs of the Times, May 11, 1904.
Jumatatu
Novemba 11
2. KUKUZA MTAZAMO BORA
a. Ni karipio gani kali linalotolewa kwa wale walio wakali kwa wengine huku wakikataa kukiri makosa yao wenyewe? Mhubiri 7:20; Yakobo 3:2 (sehemu ya kwanza).
“Je hamtatambua mapungufu yenu wenyewe na kuvaa silaha zote za haki? Je, hutakuwa macho na kukosoa sana roho na tabia zako na maneno yako kama vile ulivyo juu ya wengine, ili Mungu asije akavunjiwa heshima, na ukweli wake ukawakilishwa vibaya? Utambuzi wako ungeboreshwa sana ikiwa ungefanya hivi. Kweli, neno lililo hai, lingekuwa kama moto uliofungwa katika mifupa yako, ambao ungeangaza kwa uwazi, utofauti usio na shaka kumuakilisha kristo kwa ulimwengu….
“Je hakuna hata mmoja wa wale ambao wamejifanya wapelelezi kuona mwelekeo wa nafasi ambayo wamechukua katika kujaribu kuwadhibiti nguvu? Macho yao safi ya kiroho yalikuwa wapi? Kwa nini wangeweza kutambua kibanzi kwenye jicho la ndugu, na boriti kwenye jicho lao wenyewe? ”—Testimonies to Ministers, pp. 295, 296.
b. Ni nini kinachoonyesha kwamba mtu amefikia kiwango cha ukamilifu wa kimaadili na ni jinsi gani pekee hii inawezekana? Yakobo 3:2; 1 Wakorintho13:5 (nusu ya pili).
“Ambapo ulimi usiodhibitiwa hupata nafasi ya kufanya kazi yake isiyo takatifu furaha ya Bwana haiwezi kudumu.
“Watu wenye kutia shaka, wanaowawazia na kuwasema vibaya ndugu zao, wakumbuke kwamba wanafanya mambo ya shetani. Hebu kila mshiriki wa kanisa afanye kazi kwa dhamira ya dhati, na kwa maombi kwa ajili ya usaidizi, kuponya mshiriki mgonjwa, kila mmoja ajisikie kuwa ni wajibu na upendeleo wake kupitisha tofauti ndogo na makosa bila maoni. Usikuze makosa madogo yaliyofanywa na mtu fulani, lakini fikiria wema ulio ndani yake. Kila wakati makosa haya yanafikiriwa na kuzungumzwa, yanakuwa makubwa. Mlima umetengenezwa kwa kilima cha mole. Hisia mbaya na ukosefu wa kujiamini ndiyo tokeo. ”—Australasian Union Conference Record, April 15, 1903.
“Weka agano na Mungu kwamba Mtu yeyote asipokosea kwa neno, huyo ni mtu mkamilifu, na awezaye kuutawala mwili wote pia.” Yakobo 3: 2. Kumbuka kwamba maneno ya kulipiza kisasi hayamfanyi mtu ahisi kwamba amepata ushindi. Hebu Kristo azungumze kupitia kwako. Usipoteze baraka inayotokana na kutokuwaza ubaya wowote”—Testimonies for the Church, vol. 7, p. 243.
Jumanne
Novemba 12
3. INAANZIA KWENYE MZIZI
a. Fuatilia mwelekeo usiofaa unaofuata pindi tunapokaa na kinyongo, na ueleze njia peke ya kuepuka hili. Waebrania 12:15; Yakobo 3:3–5.
“Umehifadhi chuki yako dhidi ya mumeo na wengine ambao wamekukosea, lakini umeshindwa kugundua ni wapi umekosea na kuzidisha hali kwa njia yako mbaya. Roho yako imekuwa kali dhidi ya wale ambao wamekutenda udhalimu, na hisia zako zimepatikana kwa lawama na lawama. Hii inaweza kutoa afueni ya muda kwa moyo wako ulioelemewa, lakini imeacha kovu la kudumu juu ya nafsi yako. Ulimi ni kiungo kidogo, lakini umesitawisha matumizi yake yasiyofaa mpaka imekuwa moto uteketezao.
“Vitu hivi vyote vimependa kuangalia maendeleo yako ya kiroho. Lakini Mungu anaona jinsi ilivyo ngumu kwako kuwa mvumilivu na mwenye kusamehe, na anajua jinsi ya kuhurumia na kusaidia. Anahitaji wewe kurekebisha maisha yako, kurekebisha kasoro zako. Anatamani kwamba roho yako thabiti, isiyoyumba itawaliwe na neema Yake. Unapaswa kutafuta msaada wa Mungu, kwa sababu unahitaji amani na utulivu badala ya dhoruba na mabishano. Dini ya Kristo inakuamuru uache kidogo kutenda mambo kwa msukumo/mihemko, na zaidi kutoka kwa sababu iliyotakaswa na hukumu tulivu. ”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 139.
b. Kipi tunapaswa kukitambua kuhusu maneno tunayo tamka? Yakobo 3:6.
“Maneno yako yatatangaza, matendo yako yataonesha, wapi ilipo hazina yako”—Ibid., vol. 1, pp. 698, 699.
“Dada F anasukumwa na mhemko, na kutafuta makosa, na amekuwa na mengi ya kusema dhidi ya ndugu na dada zake. Hii itasababisha machafuko katika kanisa lolote. ”—Ibid., vol. 2, p. 51.
“Hebu wale wanaofurahi kufuatilia maneno ya uongo na uzushi dhidi ya watumishi wa Kristo wakumbuke kwamba Mungu ni shahidi wa matendo yao. Mguso wao wa kashfa hautii unajisi vyombo visivyo na roho bali tabia za wale ambao Kristo amewanunua kwa damu Yake. Mkono uliowafuata wahusika kwenye kuta za ikulu ya Belshaza unaweka rekodi ya uaminifu ya kila tendo la dhuluma au uonevu unaofanywa dhidi ya watu wa Mungu.”—Ibid., vol. 5, pp. 244, 245.
Jumatano
Novemba 13
4. HATA IKITOKEA KUWA NI UKWELI. . .
a. Ni maombi gani yenye nguvu yanayotolewa kuhusu mwelekeo hatari unaoenea katika siku zetu? Zaburi 15:1–3; 1 Wakorintho 13:6.
“Ulimi unaofurahia ufisadi/hila, ulimi unaobwabwaja na kusema, Taarifu/ripoti, na mimi nitaitaarifu/nitaripoti, umeelezwa na mtume Yakobo kuwa umeandaliwa kwa moto wa jehanamu. Unatema cheche za moto kila upande. Anajali kwa kiasi gani mteja wa uvumi kwamba anawachafua wasio na hatia? Haiachi shuguli yake mbaya, ingawa anaharibu matumaini na ujasiri wa wale ambao tayari wamezama chini ya mizigo yao. Anajali tu kuiendekeza tabia yake ya kupenda kashfa. Hata wale wanaojiita Wakristo hufumba macho yao katika kila kilicho safi, cha uaminifu, kilicho bora, na cha kupendeza, na kufanyia kazi kile ambacho ni kibaya na cha kuchukiza, na kukichapisha/kukitangaza ulimwenguni.
“Ninyi wenyewe mmemfungulia milango Shetani aingie. Mmempatia nafasi ya heshima katika upelelezi wenu, au mikutano ya uchunguzi. Lakini hamjaonyesha heshima kwa tabia bora iliyoanzishwa kwa miaka mingi ya uaminifu. Lugha za wivu, za kulipiza kisasi zimefanya vitendo na misukumo kwa rangi zanazokidhi maoni yao wenyewe. Wameifanya nyeusi ionekane ni nyeupe, na nyeupe iwe nyeusi. Wakati ilipopingwa kwa matamshi yao, wengine wamesema: ”Ni kweli.” Je, kukubali kwamba yaliyosemwa ni ya kweli kunahalalisha njia yenu? Hapana, hapana. Ikiwa Mungu atachukua mashtaka yote ambayo kwa kweli yanaweza kuletwa dhidi yenu, na kuyafanya kuwa mjeledi wa kuwaadhibu, vidonda vyenu vitakuwa vikubwa, na vilivyochimbika zaidi na zaidi kuliko vile ambavyo mmempatia ndugu -----.angekuwa yale yote ambayo mnamwakilisha kuwa, ambayo najua hayuko hivyo, mwenendo wenu bado isingepata udhuru.
“Tunaposikiliza shutuma dhidi ya ndugu zetu, tunachukua shutuma hizo………. [Zaburi 15:1–3 Imenukuliwa.]”—Testimonies for the Church, vol. 5, pp. 57, 58.
b. Katika dhambi saba zilizotajwa kuwa machukizo kwa Bwana, ni ngapi zinazohusika na maneno yetu? Mithali 6:16–19.
Alhamisi
Novemba 14
5. SILAHA INAYO JERUHI
a. Jinsi gani na kwa nini ni lazima tuepuke mazoea ya kawaida sana ya kusengenya? Ayubu 6:24; Mithali 11:13; 26:20–22.
“Ulimwengu wa uvumi/umbeya ungekuwa kama kila mtu angekumbuka kuwa wale wanaomwambia makosa ya wengine watayatangaza pia makosa yake kwa uhuru wakipata fursa nzuri. Tunapaswa kujitahidi kuwafikiria vizuri watu wote, hasa ndugu zetu, hadi tutakapolazimika kufikiria vingine. Hatupaswi kutoa taarifa mbaya kwa haraka. Mara nyingi hizi ni matokeo ya wivu au kutokuelewana, au zinaweza kuendelea kutokana na kutia chumvi mambo kuuelewa ukweli kwa juu juu tu. Punde wivu na tuhuma zinapopata nafasi, zitapandikiza matangazo yao yatakayopeperushwa kama upepo. Endapo ndugu ameiacha njia, basi huo ndio wakati wa kuionesha nia yako ya Kweli kwake. Nenda kwake kwa wema, omba naye na kwa ajili yake, ukiikumbuka gharama isiyo na kipimo ambayo Kristo ameilipa kwa ajili ya ukombozi wake. Kwa njia hii unaweza kuokoa roho kutoka mautini, na kuficha wingi wa dhambi.
“Kutazama, kutamka neno, au hata lafudhi ya sauti, vinaweza kujaa uongo, vikizama kama mshale ndani ya moyo, na kusababisha jeraha lisilopona. Kwa hiyo shaka, aibu, vinaweza kutupwa juu ya yule ambaye kupitia kwake Mungu angefanya kazi nzuri, na ushawishi wake unakuwa umeathirika, umuhimu wake umeharibiwa. Miongoni mwa baadhi ya makundi ya wanyama, ikiwa mmoja wao amejeruhiwa na kuanguka, mara moja huwekwa chini na kuraruliwa na wenzake. Roho hiyo hiyo ya kikatili inaendekezwa na wanaume na wanawake wanaolibeba jina la Wakristo. Wanaonyesha bidii ya kifarisayo kwa kuwapiga mawe wengine wasio na hatia kuliko wao. Kuna wengine ambao wanaelekeza makosa na kushindwa kwa wengine ili wageuze umakini kutoka dhambi zao, au wapate sifa ya juhudi kubwa kwa Mungu na kanisa.”—Testimonies for the Church, vol. 5, pp. 58, 59.
“Wakati ambao mara nyingi ni mbaya zaidi kuliko kupotezwa katika uvumi usiofaa, ujinga, na uovu unapaswa kutolewa kwa vitu vya juu na vyenye heshima.”—Ibid.,p. 176.
Ijumaa
Novemba 15
MASWALI TAFAKARI BINAFSI
1. Kwa nini nipunguze tabia ya kuwa na maoni juu ya kila kitu.
2. Taja kipengele muhimu cha tabia kama ya Kristo ambayo mara nyingi hupuuzwa.
3. Tunapowadharau waumini wenzetu mbele ya wengine, Mungu huonaje jambo hilo?
4. Ninahitaji kujifunza nini kutokana na Zaburi ya 15 na kwa nini ni muhimu?
5. Ninawezaje kuwa na hatia ya kupanda mafarakano kati ya ndugu na kwa nini ni lazima kuacha?