Jumapili
Septemba 29
1. WANAFUNZI WA KRISTO
a. Watu watatu walioitwa “Yakobo” ambao walihusishwa na kristo walikuwa nani na ni yupi tunayemwona kwa kawaida? Mathayo 10:2, 3; 13:55.
b. Taja nyakati maalum na Yesu ambazo Yakobo, ndugu yake Yohana, alipitia. Luka8:51–55;Mathayo17:1,2;Marko14:32–34.
“Yohana, mwana wa Zebedayo, alikuwa mmoja wa wanafunzi wawili wa kwanza kumfuata Yesu. Yeye na kaka yake Yakobo walikuwa wamekuwa miongoni mwa kundi la kwanza la watu waliokuwa wameacha vyote kwa ajili ya kumtumikia. Kwa furaha walikuwa wameziacha nyumba na marafiki kusudi wawe naye; walikuwa wametembea na kuzungumza naye, walikuwa wamekuwa naye mahali pa faragha, na katika mikusanyiko ya hadhara. Alikuwa ameondosha hofu zao, akawaokoa na hatari, akatuliza maumivu yao, akafariji huzuni zao, na kwa uvumilivu na upendo akawafundisha, hadi mioyo yao ikaonekana kama vile imeunganishwa naye, na katika hisia za upendo wao walitamani kuwa karibu zaidi naye katika ufalme wake. ”—The Desire of Ages, p. 548.
“Karibu na mahali pa kuingilia bustanini, Yesu aliwaacha wanafunzi pale isipokuwa watatu, akiwataka wajiombee na kumwombea na Yeye. Aliingia katika faragha za bustani ile akiwa pamoja na Petro, Yakobo na Yohana. Hawa watatu walikuwa watu wa karibu sana wa Kristo.… sasa katika pambano lake kuu, Yesu alitaka wawe karibu yake. Mara nyingi walikuwa naye usiku mzima mahali hapa. Katika nyakati hizo, ”—Ibid., p. 686.
Jumatatu
Septemba 30
2. KUNYWEA KIKOMBE
a. Elezea lengo la awali la Yakobo, mwana wa Zebedayo, pamoja na ndugu yake, Yohana. Marko 10:35–38.
“Katika kila nafasi iliyowezekana, Yohana alikuwa katika nafasi iliyofuata baada ya Mwokozi, na Yakobo alitamani kuheshimiwa kwa kuwa karibu sana na Mwokozi.
“Mama yao alikuwa mfuasi wa Kristo, na alikuwa amemhudumia kwa vitu vyake bure. Akiwa na upendo wa umama na shauku kwa wanawe, alitamani wapate nafasi ya juu katika ufalme ule. Aliwahamasisha waombe jambo hilo.
“Mama na wanawe hao kwa pamoja walikuja kwa Yesu, wakiomba kwamba awape ruhusa waomba kile mioyo yao ilichotaka kuomba.
”Mwataka niwafanyie nini?” Aliuliza.
Mama akajibu, ”Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.”
“Yesu akawavumilia kwa upendo, pasipo kukemea ubinafsi wao kwa kile kitendo chao cha kutafuta upendeleo zaidi ya ndugu zao wengine. Alisoma mioyo yao, akajua kina cha mafungamano yao na Yeye. Upendo wao si wa kibinadamu tu; ingawa wamenajisiwa na mambo ya kidunia ya njia za kibinadamu, upendo wao ule unatiririka kutoka katika chemchemi ya upendo wake uokoao. Hataki kukemea, bali kuwaongezea kina na kuwafanya kuwa safi. Alisema, ”Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?”
Wakakumbuka maneno yake ya fumbo, yaliyokuwa yakielekeza kwenye majaribu na mateso yake, lakini bado wanajibu kwa kujiamini, ”Twaweza.” Walihesabu kama ni kuonyesha heshima kubwa kwa kuthibitisha utii wao kwake katika kushiriki mambo yote yatakayompata Bwana wao.
”Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa,” alisema; mbele yake kukiwa na msalaba badala ya kiti cha enzi, na wanyang’anyi wawili ndio wangekuwa naye upande wake wa kulia na wa kushoto. ”—The Desire of Ages, pp. 548, 549.
b. Kama vile kristo alivyokuwa ametabiri, ni nini kiliwapata Yakobo na ndugu yake, Yohana, baada ya kupaa kwa Bwana? Matendo12:1, 2; Ufunuo 1:9.
“Yohana na Yakobo wangeshiriki mateso ya Bwana wao, mmoja, akiwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wote kufa kwa upanga; na mwingine, mtu aliyepitia masumbufu, mashutumu na mateso.”—Ibid., 549.
Jumanne
Oktoba 1
3. NANI ALIANDIKA WARAKA HUO?
a. Uvuvio unaelezeaje Yakobo, mwana wa Alfayo - mmoja wa wale kumi na wawili (lakini si Zebedayo ndugu wa Yohana)? Marko 15:40.
“Kulikuwa na Mlawi Mathayo mtoza ushuru, aliyeitwa kutoka katika maisha ya shughuli za biashara, na kutii Rumi; Simoni mwenye bidii, adui asiyebadilika na mamlaka ya kifalme; msukumo unaojitosheleza, uliwachangamsha Petro pamoja na Andrea ndugu yake; Yuda Myahudi, aliyepambwa, mwenye uwezo, na mwenye roho mbaya; Filipo na Tomaso walikuwa waaminifu na wenye bidii, lakini wenye mioyo mizito kuamini; Yakobo mdogo na Yuda, ambao hawakuwa mashuhuri kati ya ndugu, lakini ni watu wa nguvu, wenye msimamo mzuri katika makosa yao na Katika fadhila zao; Nathanael, mtoto mwenye unyofu na uaminifu; na wana wa Zebedayo wenye kutaka makuu, wenye mioyo ya upendo.”—Education, pp. 85, 86.
b. Kwa nini kuna uwezekano kwamba mwandishi wa waraka wa Yakobo (anayejulikana kama mtume kwani alimjua Bwana ana kwa ana) angekuwa ndugu wa kambo wa Kristo na maelezo yake mwenyewe yanaonyeshaje kwamba tabia yake ilikuwa imebadilishwa na ushawishi wa Bwana? Yakobo 1:1 (nusu ya kwanza).
“Kristo hakueleweka na ndugu zake; kwani hakuwa kama wao. Alifanya kazi kutuliza kila kisa cha mateso alichoona, na kila wakati alifanikiwa. Alikuwa na pesa kidogo za kutoa, lakini mara nyingi alitoa chakula chake cha unyenyekevu kwa wale ambao alifikiria kuwa wahitaji zaidi kuliko yeye mwenyewe. Ndugu zake walihisi kwamba mvuto wake ulikwenda mbali ata kuingilia mvuto wao; kwani walizungumza kwa ukali kwa masikini, na roho zilizo dhalilishwa, Kristo aliwatafuta hawa, na akasema maneno ya kutia moyo kwao. Ikiwa wakati wa mzunguko wa familia, hakuweza kufanya chochote zaidi, angeweza kimya kimya na kwa siri iwezekanavyo, kuwapa viumbe wanyonge ambao alikuwa akijaribu kuwasaidia, kikombe cha maji baridi, na kisha kuweka chakula chake mwenyewe mikononi mwao. ”—This Day With God, p. 59.
c. Paulo alionyeshaje heshima yake kwa Yakobo, ndugu wa Yesu, Wagalatia1:17–19; Matendo21:18.
Jumatano
Oktoba 2
4. KUFAFANUA BAADHI YA MATATIZO
a. Ni nini kinachoonyesha kwamba Yakobo, ndugu wa Kristo, alikuwa mtu mwenye ushawishi katika baraza muhimu katika kanisa la awali? Matendo 15:5, 6, 13, 19, 20.
“Kwa mfano huu Yakobo anaonekana kuchaguliwa kuwa ndiye atangaze uamuzi uliofikiwa na baraza. Ilikuwa ni hukumu yake kwamba ni sheria, na hasa sheria ya tohara, isihimizwe juu ya Mataifa, au hata kupendekezwa kwao. Yakobo alitaka kuvutia akili za ndugu zake na ukweli kwamba, katika kumgeukia Mungu, watu wa Mataifa walikuwa wamefanya badiliko kubwa katika maisha yao na kwamba tahadhari nyingi zitumike ili wasiwasumbue kwa maswali yenye kutatanisha na mashaka ya umuhimu mdogo, wasije wakakata tamaa katika kumfuata Kristo. ”—The Acts of the Apostles, p. 195.
b. Madai gani ya kawaida lakini yenye makosa yanakanushwa na jukumu kuu la Yakobo katika baraza hili muhimu? Mathayo 16:18.
“Yakobo aliongoza baraza, na uamuzi wake wa mwisho ulikuwa, ‘kwa hiyo hukumu yangu ni, tusiwasumbue hao watu wa Mataifa wamemgeukia Mungu.’
“Hii ilimaliza mjadala. Katika tukio hili tunakanusha fundisho lililoshikiliwa na Kanisa Katoriki la Roma kwamba Petro alikuwa mkuu wa Kanisa. Wale ambao, wakiwa mapapa, wamedai kuwa waandamizi wake hawana msingi wa kimaandiko wa kujidai kwao. Hakuna kitu katika maisha ya Petro yanatoa kibali kwa dai kwamba aliinuliwa juu ya ndugu zake kama makamu aliye juu zaidi. Ikiwa wale waliotangazwa kuwa warithi wa Petro walikuwa wamefuata mfano wake, siku zote wangeridhika kubaki katika usawa na ndugu zao. ”—Ibid., pp. 194, 195.
“Mwokozi hakuikabidhi kazi ya injili kwa Petro kama mtu binafsi. Wakati fulani baadaye, alirudia maneno yale aliyoambiwa Petro akiyatumia kwa kanisa. Kitu kile kile kilisemwa kwa wale kumi na wawili kama wawakilishi wa jamii ya waamini. Ikiwa Yesu alikuwa amekasimisha madaraka rasmi yoyote kwa mmoja wa wanafunzi wake, tusingetarajia kuwakuta mara kwa mara wakibishana kuhusu nani awe mkubwa wa wote. Wangetii matakwa ya Bwana wao, na kumheshimu yeye ambaye alimchagua. ”—The Desire of Ages, p. 414.
Alhamisi
Oktoba 3
5. ISRAELI YA MUNGU
a. Waraka huu umeandikwa kwa nani na unawahusishaje wote wanaomkubali Yesu kuwa Bwana? Yakobo 1:1 (nusu ya pili); Wagalatia 3:27–29.
“Miongoni mwa Israeli ya Mungu wangehesabiwa wengi ambao hawakuwa wazao wa Abrahamu kwa jinsi ya kimwili. ”—Prophets and Kings, p. 367.
“Maisha ya Kristo yalianzisha dini ambayo ndani yake hakuna tabaka, dini ambayo kwayo Myahudi na Myunani, walio huru na wafungwa, wameunganishwa katika udugu wa pamoja, sawa mbele za Mungu.”—Testimonies for the Church, vol. 9,p. 191.
“Ukristo hufanya kifungo chenye nguvu cha muungano kati ya bwana na mtumwa, mfalme na mtawaliwa, mhudumu wa mwinjilisti na mdhambi aliyedhalilishwa ambaye amepata kutakaswa dhambi zake katika kristo.”— The Acts of the Apostles, p. 460.
b. Katika unabii, ni jina gani linalopewa Israeli ya mwisho wa kiroho na uzoefu wao unaelezwaje kabla tu ya kurudi kwa Kristo? Ufunuo 7:4.
“Mara tulisikia sauti ya Mungu kama ya maji mengi, iliyotujulisha siku na saa ya kuja kwa Yesu. Watakatifu walio hai, 144,000 kwa idadi yao, waliifahamu na kuielewa sauti, wakati waovu wakidhani ni radi na tetemeko la ardhi….
“144,000 wote walikuwa wamepigwa mihuri na wameunganishwa kikamilifu. Kwenye paji la uso wao palikuwa na maneno Mungu, Yerusalemu Mpya, na nyota tukufu iliyo na jina jipya la Yesu. Katika hali yetu ya furaha na takatifu waovu walikuwa wamekasirika, na walitamani kutukimbilia ili watukamate na kututia gerezani, ambapo tulinyosha mkono kwa jina la Bwana, na wakaanguka chini bila msaada wowote. Ndipo sinagogi la Shetani likatambua kwamba Mungu alikuwa ametupenda sisi ambao tungeweza kuoshana miguu, na kuwasalimu ndugu kwa busu takatifu, hivyo wakaabudu miguuni mwetu.”—Testimonies for the Church, vol. 1, p. 59.
Ijumaa
Oktoba 4
MASWALI TAFAKARI BINAFSI
1. Yakobo, mwana wa Zebedayo, alikuaje akawa kama kristo zaidi?
2. Yakobo, ndugu wa kambo wa Yesu, alikuaje na kuwa kama kristo zaidi?
3. Ni uthibitisho gani katika maandiko unaoonyesha kwamba Petro hakuwa mtume mkuu?
4. Paulo anaelezeaje umoja na thamani sawa ya Wkristo wote?
5. Ni nini kinachoonyesha ushindi wa mwisho kabisa wa Israeli wa roho wa mungu?