Sadaka ya Kwanza ya Sabato kwa ajili ya Makao Makuu ya Union ya Kolombia
Kolombia ni taifa lililo Amerika kusini lenye wakazi ya milioni 51. Viwandani pamoja na mafuta, viwanda, nguo, ujenzi, kilimo, benki na huduma. Kati ya wakazi 73% ya wakazi ni Wakatoliki; 9.1%wanadai kuwa dini zisizo za kikristo 6.9% ni wainjilisti, 6.5% hawana dini, 2.9% ni Waprotestanti, na 0.9 wanajitangaza kuwa hawaamini Mungu. Hali hii inawakilisha changamoto kubwa kwa kanisa la mungu hapa. katika miaka ya 1960, ujumbe wa malaika wa tatu ulifika Kolombia huku taifa hilo likiathirika kiadili kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katikati ya msukosuko huo, tulifikia washiriki wapatao 100 kufikia mwaka wa 1971 wakati kanisa liliposajiliwa rasmi. Siku hizo wafanyakazi walikuwa wachache, lakini hawakukosa kamwe ujasiri na juhudi ya kutoa kila kitu kwa ajili ya kazi waliyoipenda. Sikuzote tutathamini utegemezo wa wachungaji na wahudumu ambao, wakiacha nchi zao na faraja, walikuja kwa shangwe kutegemeza kazi katika Kolombia—wakijitoa wenyewe kwa moyo wote kueneza ujumbe hapa.
Kwa neema ya Mungu, mwaka 2006, Union ya Kolombia ilipangwa, na leo ina Field tatu. Makao makuu ya Union yako katika eneo la vijijini manispaa ya Barbosa, Santander.
Ili kutumikia ndugu zetu na wale wanaopendezwa zaidi na kweli, tunaona uhitaji wa haraka wa kupanua majengo yaliyopo leo. Hivi sasa, tuna shamba ambapo ofisi zetu, shule za wamishonari na idara ya vyombo vya habari inafanya kazi. Hapa pia tunaandaa makongamano, semina, na mapumziko ya kiroho kwa washiriki wetu na wale wapya wanaopendezwa na ujumbe.
Sehemu ya miundombinu tayari imejengwa kwenye mali hii, na vifaa vya ziada vinaendelea kwa sasa, lakini, tunakosa rasilimali za kuzimaliza. Ndiyo maana tunaomba ukarimu wa kanisa la kifamilia duniani kote. Usaidizi wa matoleo yako ya ukarimu utaturuhusu kuwa na vifaa vinavyofaa zaidi kuhudumia roho zilizo na njaa ya maarifa ya Bwana.
Tunathamini sana michango yako. Milele pekee ndiyo itaweza kuonyesha ni kiasi gani michango na matoleo yako yatakuwa yamefanya.
Ndugu na dada zako kutoka Union ya kolombia