Back to top

Sabbath Bible Lessons

Masomo katika Waraka wa Yakobo

 <<    >> 
Somo la 11 Sabato, Desemba 14, 2024

Kufuata Mwonekano Mnyenyekevu

FUNGU LA KUKARIRI: “Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza. ” (Yakobo 4:10).

“Tunapofuata njia ya unyenyekevu ya utiifu, tunaacha njia angavu ya kuelekea mbinguni kwa wengine kutembea ndani yake. Ni fursa yetu kuwa na uzoefu wa kina zaidi katika mambo ya Mungu.”—The Signs of the Times, March 17, 1890.

Inapendekezwa kusoma:   Testimonies for the Church, vol. 2, pp. 41-44, vol. 2, pp. . 

Jumapili Desemba 8

1. KUEPUKA UTAMBUZI WA UONGO

a. Ni tabia gani mbaya sana inayohitaji kuachwa na wote wanaodai kuwapenda ndugu zao, na kwa nini? Yakobo 4:11, 12 .

“Haipaswi kuchukuliwa kuwa jambo jepesi kuwasema vibaya wengine au kujifanya waamuzi wa nia au matendo yao.”—Patriarchs and Prophets, p. 385.

“Thamani ya kweli ya maadili haitafuti kujitengenezea nafasi kwa kufikiria na kusema maovu, kwa kuwashusha thamani wengine. Wivu wote, matukano yote, pamoja na kutokuamini kote, lazima viondolewe mbali na watoto wa Mungu.”— Our High Calling, p. 234.

“Juhudi za dhati zinapaswa kufanywa katika kila kanisa katika kuondoa kuzungumza maovu na roho ya ukosoaji miongoni mwa washiriki kama dhambi zinazozaa maovu makubwa zaidi ndani ya kanisa. Ukali na kutafuta makosa lazima vikemewe kama kazi za Shetani. Upendo na ujasiri wa pande zote lazima uhimizwe na kuimarishwa kwa washiriki wa kanisa. Hebu wote, kwa kumcha Mungu na kwa upendo kwa ndugu zao, wazibe masikio yao dhidi ya masengenyo na mashutumu. Mwelekezeni mchonganishi au mleta habari (nipashe) kwenye mafundisho ya Neno la Mungu. Mwambieni ayatii Maandiko na apeleke malalamiko yake moja kwa moja kwa wale anaofikiria kuwa wamekosea. Hatua hii ya umoja ingeleta mafuriko ya nuru ndani ya kanisa na kufunga mlango wa mafuriko ya uovu. Hivyo Mungu atatukuzwa, na roho nyingi zitaokolewa. ”—Testimonies for the Church, vol. 5, pp. 609, 610.


Jumatatu Desemba 9

2. KUCHUKULIA NURU KWA UZITO

a. Tunapofanya mipango, tunahitaji kukumbuka nini kila mara? Zaburi 16:8; Yakobo 4:10, 13–16 .

“Jiweke wakfu kwa Mungu asubuhi; fanya hii iwe kazi yako ya kwanza kabisa. Maombi yako na yawe, ‘Nichukue, Ee Bwana, kuwa wako kabisa. Ninaweka mipango yangu yote miguuni pako. Nitumie leo katika huduma Yako. Kaa nami, na kazi yangu yote itekelezwe ndani yako.’ Hili ni jambo la kila siku. Kila asubuhi jiweke wakfu kwa Mungu kwa ajili ya siku hiyo. Peleka mipango yako yote Kwake, ili itekelezwe au uiache kama vile riziki Yake itakavyoonyesha. Hivyo siku baada ya siku unaweza kuwa unayatoa maisha yako mikononi mwa Mungu, na hivyo maisha yako yatafinyangwa zaidi na zaidi baada ya maisha ya Kristo.”—Steps to Christ, p. 70.

b. Elezea wajibu mzito na uwajibikaji tulionao kila mmoja wetu kwa nuru ya mbinguni inayotolewa kwetu katika nyanja zote za maisha. Yakobo 4:17; Mathayo 12:31, 32 .

“Si Mungu anayepofusha macho ya watu na kuifanya mioyo yao kuwa migumu. Yeye huwapelekea nuru ili kusahihisha makosa yao, na kuwaongoza katika njia salama; macho yao hupofushwa na mioyo yao kufanywa migumu kwa sababu ya wao kuikataa nuru hiyo. Mara nyingi hali hii hutokea taratibu, na kama vile pasipo kuonekana. Nuru huja moyoni kwa njia ya neno la Mungu, kupitia watumishi wake, au kupitia kazi za moja kwa moja za Roho wake; lakini pale hata mshale mmoja wa nuru unapopuuzwa, kunakuwa na sehemu ya uhafifisho wa uelewa wa kiroho, na udhihirisho wa pili wa nuru huonekana kwa uwazi uliopungua. Hivyo giza huongezeka, mpaka kunapokuwa usiku moyoni. ”— The Desire of Ages, p. 322.

“Ni hatari kubwa kutamka neno ulilo na mashaka nalo, hatari ya kuhoji na kukosoa nuru ya kimbingu. Mazoea ya kupinga pasipo uangalifu na heshima huathiri tabia, na huelekeza katika utovu wa heshima na kutoamini. Watu wengi wanaokuwa na mazoea haya wameendelea hivyo pasipo kutambua hatari iliyopo, mpaka walipokuwa katika hali ya kupinga na kukataa kazi ya Roho Mtakatifu. ”—Ibid., p. 323.

“Watu wanapozungumziwa kuhusu afya, mara nyingi husema: „Tunajua mengi zaidi kuliko tunavyofikiri.” Hawatambui kwamba wanawajibika kwa kila miale ya nuru kuhusiana na ustawi wao wa kimwili, na kwamba kila tabia yao iko wazi kwa ukaguzi wa Mungu. ”—Testimonies for the Church, vol. 6, p. 372.


Jumanne Desemba 10

3. UTAJIRI KUPITA KIASI

a. Ni maonyo gani yanatolewa kuhusiana na majaribu yanayo wazunguka wale walio barikiwa mali nyingi kuliko wengine? Yakobo 5:1.

“Wachungaji hawapaswi kutumia maneno ya kusifia au kuwapendelea watu. Kumekuwa na hatari kubwa ya kukosea hapa, na bado ipo, ya kufanya tofauti kidogo na matajiri, au kuwabembeleza kwa umakini maalum, ikiwa sio kwa maneno. Kuna hatari ya „kupendezwa na watu” kwa sababu ya faida, lakini kwa kufanya hivyo masilahi yao ya milele yako hatarini. Mchungaji anaweza kuwa kipenzi maalum cha mtu tajiri, na anaweza kuwa huru sana pamoja naye; hii humtukuza mchungaji, na yeye pia humwaga sifa juu ya fadhili za mfadhili wake. Jina lake linaweza kuinuliwa kwa kuonekana kwenye chapisho, na bado mfadhili huyo huria anaweza kuwa hafai kabisa sifa aliyopewa. Ukarimu wake haukutokana na kanuni ya kina, inayoishi ya kutenda mema na mali zake, kuendeleza kazi ya Mungu kwa sababu aliithamini, bali ulitoka katika nia ya ubinafsi, hamu ya kufikiriwa kuwa ni mkarimu. Anaweza kuwa ametoa kutoka kwa msukumo, lakini ukarimu wake hauna kina cha kanuni. Anaweza kusukumwa na kusikiliza ukweli wenye kuchochea ambao kwa muda huo ulifungua kamba zake za mkoba; lakini, baada ya yote, ukarimu wake hauna nia ya kina. Anatoa kwa kujionesha; mkoba wake unafunguliwa kimkakati na hufungwa salama kimkakati. Hastahili pongezi, kwa maana yeye kwa kila hali na neno ni mtu bahili na asipoongoka kabisa, mkoba wake na vyote vitasikia kemeo linalokausha: „Nendeni sasa, enyi matajiri, kulia na kuomboleza kwa ajili ya huzuni zitakazo kuja juu yenu . Utajiri wako umeharibika, na mavazi yako yameliwa na nondo. Hao wataamka mwishowe kutoka kwa udanganyifu wa kutisha. Wale ambao walisifu ukarimu wao maonesho walimsaidia Shetani kuwadanganya na kuwafanya wafikiri kwamba walikuwa wakarimu sana, wenye kujitolea sana, wakati hawakujua kanuni za kwanza za ukarimu au kujitolea”—Testimonies for the Church, vol. 1, pp. 475, 476.

b. Tutaboresha vipi vipaumbele vyetu kuhusu pesa? Mithali 11:4 .

“Kwa kutenda, ukarimu hupanua na kuimarisha, mpaka inakuwa kanuni nakutawala ndani ya nafsi. Ni hatari sana kwa roho kuruhusu ubinafsi na uchoyo vipate nafasi hata ndogo moyoni. ”—Ibid., vol. 3, pp. 548, 549.


Jumatano Desemba 11

4. KUACHA SANAMU

a. Ni nini mara nyingi sababu ya watu kupata utajiri? Yakobo 5:2 (sehemu ya kwanza).

“Katika kizazi hiki hamu ya kupata faida ni shauku kuu. Utajiri mara nyingi hupatikana kwa ulaghai. Kuna watu wengi wanaohangaika na umaskini, wanalazimika kufanya kazi kwa bidii kwa ujira mdogo, hawawezi kupata hata mahitaji duni ya maisha. Taabu na kunyima, bila matumaini ya mambo bora, hufanya mzigo wao kuwa mzito. Wakiwa wametunzwa na kudhulumiwa, hawajui waelekee wapi kupata nafuu. Na haya yote ili matajiri waunge mkono ubadhirifu wao au watimize tamaa yao ya kulimbikiza!

“Kupenda pesa na kujionyesha kumeifanya dunia hii kuwa pango la wezi na wanyang’anyi. Maandiko huonyesha uchoyo na uonevu utakaokuwapo kabla tu ya kuja kwa Kristo mara ya pili.”— Prophets and Kings, pp. 650, 651.

b. Ni nini kinachochochea sehemu kubwa ya ulimwengu leo—na ni mwito gani unaohitaji kufanywa kwa wale wanaoongozwa nao? 1 Timotheo 6:9, 10; Kumbukumbu la Torati 8:18, 19 .

“Biblia haimlaumu mtu kwa kuwa tajiri, ikiwa amepata utajiri wake kwa uaminifu. Sio pesa, bali kupenda pesa, ndio chanzo cha maovu yote. Mungu ndiye awapaye wanadamu uwezo wa kupata mali; na mikononi mwa yule anayetenda kama wakili wa Mungu, akitumia mali yake bila ubinafsi, mali ni baraka, kwa aliye nayo na kwa ulimwengu pia. Lakini wengi, wakiwa wamezama katika kupendezwa kwao na hazina za kilimwengu, wanakuwa wasiojali madai ya Mungu na mahitaji ya wanadamu wenzao. Wanachukulia mali zao kama njia ya kujitukuza. Wanaongeza nyumba kwa nyumba, na ardhi kwa ardhi; wanazijaza nyumba zao anasa, huku wote wanaowazunguka ni wanadamu katika taabu na uhalifu, katika magonjwa na kifo. Wale wanaotoa maisha yao kwa kujitanguliza wenyewe wanasitawisha ndani yao wenyewe, si sifa za Mungu, bali sifa za yule mwovu.

“Watu hawa wanahitaji injili. Wanahitaji kugeuzwa macho yao kutoka kwenye ubatili wa vitu vya kimwili ili kutazama thamani ya utajiri wa kudumu. . . .

”Wengine wamefaa kufanya kazi kwa madarasa ya juu. Hawa wanapaswa kutafuta hekima kutoka kwa Mungu ili kujua jinsi ya kuwafikia watu hawa, wasiwe na mazoea ya kawaida tu nao, bali kwa juhudi binafsi na imani iliyo hai ili kuwaamsha wapate mahitaji ya nafsi, ili kuwaongoza kwenye ujuzi wa ukweli. kama ilivyo ndani ya Yesu.”—The Ministry of Healing, pp. 212, 213.


Alhamisi Desemba 12

5. KUANGALIA ZAIDI YA MALI

a. Elezea matokeo ya faida iliyopatikana kwa njia isiyo halali. Yakobo 5:2 (sehemu ya mwisho).

“Utajiri huleta majukumu makubwa. Kupata utajiri kwa njia isivyo haki, kwa hila katika biashara, kwa kumwonea mjane na yatima, au kwa kujilimbikizia mali na kupuuza mahitaji ya mhitaji, mwishowe italeta adhabu ya haki iliyoelezewa na mtume aliyevuviwa.”—Testimonies for the Church, vol. 2, p. 682.

b. Je, ni ujumbe gani maalum wa Mungu kuhusu utajiri? 1 Timotheo 6:17–19.

“Wanyenyekevu na maskini zaidi wa wanafunzi wa Kweli wa Kristo, ambao ni matajiri wa matendo mema, wamebarikiwa zaidi na ni wa thamani mbele za Mungu kuliko watu wanaojivunia utajiri wao mwingi. Wao ni wenye heshima zaidi katika nyua za mbinguni kuliko wafalme waliotukuka sana na wakuu wasio matajiri kwa Mungu.. . . .

“Wale wanaojilimbikizia mali au kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika ardhi, wakati wakinyima familia zao faraja ya maisha, wanatenda kama watu wenye wazimu. Hawaziruhusu familia zao kufurahia vitu ambavyo Mungu amewapatia tele. Pamoja na kwamba wana mali nyingi, familia zao hulazimishwa mara kwa mara kufanya kazi zaidi ya nguvu zao kutunza mali zaidi za kujilimbikizia. Ubongo, mfupa, na misuli hutumikishwa kwa kiasi kikubwa kujilimbikizia, na majukumu ya dini na ya Kikristo yanapuzwa. Kazi, kazi, kazi, ni tamaa toka asubuhi hadi usiku.

“Wengi hawaoneshi shauku ya dhati ya kujifunza mapenzi ya Mungu na kuelewa madai Yake kwao. Wengine wanaojaribu kuifundisha Kweli kwa wengine wao wenyewe hawalitii Neno la Mungu. Zaidi kazi ya Mungu inavyokuwa na waalimu kama hao, ndivyo itakavyosonga mbele kidogo. ”— Ibid., pp. 682, 683.


Ijumaa Desemba 13

MASWALI TAFAKARI BINAFSI

1. Ninapokazia sana mapungufu ya wengine, ninafanya nini?

2. Elezea jinsi Roho Mtakatifu anahuzunishwa tunapopuuza nuru iliyotumwa na Mbingu.

3. Ni jinsi gani watu matajiri na wachungaji wao wanaweza kunaswa?

4. Kwa nini pupa inaongezeka na kwa nini tunapaswa kuiepuka sasa kuliko wakati mwingine wowote?

5. Eleza uzuri na faida za unyenyekevu katika Kristo.

 <<    >>