Back to top

Sabbath Bible Lessons

Masomo katika Waraka wa Yakobo

 <<    >> 
Somo la 6 Sabato, Novemba 9, 2024

Imani Katika Matendo

FUNGU LA KUKARIRI: “Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? ” (Yakobo 2:20).

“Ingawa matendo mema hayataokoa hata nafsi moja, lakini haiwezekani ata nafsi moja kuokolewa bila matendo.”—Faith and Works, p. 111.

Inapendekezwa kusoma:   Early Writings, pp. 226-228, 269-273. 

Jumapili Novemba 3

1. IMANI NA MFANO

a. Kwa nini ni muhimu kabisa kuishi katika upatano kamili na imani tunayokiri? 1 Wakorintho 4:9; 1 Yohana 5:3; Yakobo 2:14.

“Hebu wasiwepo watu wanaojidanganya kwa kuamini kwamba wanaweza kuwa watakatifu wakati wanavunja mojawapo ya matakwa ya Mungu kwa makusudi. Kuendekeza kutenda dhambi inayojulikana kunanyamazisha sauti ya Roho anayetushuhudia na kumtenga mtu mbali na Mungu.”—The Great Controversy, p. 472.

“Ushuhuda wa maisha ya mtu unatangaza kwa ulimwengu kama yeye ni mkweli au la na kwa imani anayokiri. Mwenendo wako unapunguza viwango vya uzito sheria ya Mungu mbele ya marafiki zako wa kidunia. Unasema kwao: “Unaweza kutii au kutotii amri. Ninaamini kwamba sheria ya Mungu, kwa namna fulani, inawabana wanadamu; lakini, baada ya yote, Bwana si mwangalifu sana kuhusu utunzaji mkali wa sheria Yake. amri, na uasi wa hapa na pale hautembelewi na ukali kutoka Kwake.

“Wengi hujitetea kwa kuivunja Sabato kwa kurejelea mfano wako. Wanabishana kwamba ikiwa mtu mwema sana kama wewe, ambaye anaamini siku ya saba ni Sabato, anaweza kujishughulisha na kazi za kilimwengu katika siku hiyo wakati hali zinapoonekana kuhitajika, bila shaka wanaweza kufanya vivyo hivyo bila kulaaniwa. Nafsi nyingi zitakukabili katika hukumu, na kufanya ushawishi wako kuwa kisingizio cha kutotii kwao sheria ya Mungu. Ingawa hii haitakuwa msamaha kwa dhambi zao, lakini hii itazungumzia kwa utisho kuhusiana na wewe. ”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 250.


Jumatatu Novemba 4

2. MBINGU NA NCHI ZINATAZAMA

a. Yakobo anatoa mfano gani ili kufafanua unafiki wa mazungumzo matupu bila matendo? Yakobo 2:15–17.

“Hotuba fasaha zaidi inayoweza kuhubiriwa juu ya sheria ya Amri Kumi ni kuzitenda. Utii unapaswa kufanywa kuwa jukumu la kibinafsi. Uzembe wa jukumu hili ni dhambi kubwa. Mungu hutuweka chini ya majukumu sio tu kujihakikishia mbingu wenyewe, lakini kuhisi ni jukumu la lazima kuwaonesha wengine njia na, kupitia utunzaji wetu na upendo usio wa kimasilahi, kuwaongoza kwa Kristo wale wanaokuja katika uwanja wa ushawishi wetu. Kukosekana kwa kanuni ambayo inabainisha maisha ya wengi wanaodai kuwa Wakristo ni ya kutisha. Kutozingatia kwao sheria ya Mungu huwavunja moyo wale wanaotambua madai Yake matakatifu na huwageuza hao kutoka kwa Ukweli ambao wangeukubali vinginevyo.”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 58. [Author’s emphasis.]

b. Imani ya kweli katika kristo inamaanisha nini? Yakobo 2:18; Mathayo 6:24.

“Mungu ameshasema, na anamaanisha hivyo hivyo kwamba mwanadamu anapaswa atii. Haulizi kama ina urahisi kwake kufanya hivyo. Bwana wa uzima na utukufu hakuangalia urahisi au radhi Yake pale alipoacha cheo Chake cha daraja la juu na kuwa Mtu wa huzuni ajuaye sikitiko, akikubali fedheha na kifo ili kumkomboa mwanadamu kutokana na matokeo ya uasi wake. Yesu alikufa, si ili amwokoe mwanadamu katika dhambi zake, bali kutoka kwa dhambi zake. Mwanadamu anapaswa kuacha upotovu wa njia zake, kufuata mfano wa Kristo, kuchukua msalaba Wake na kumfuata, kujikana nafsi, na kumtii Mungu kwa gharama yoyote.

“Ikiwa sisi ni watumishi wa Kweli wa Mungu, kusiwe na maswali akilini mwetu iwapo tutii amri Zake au kutafuta mapenzi yetu ya kimwili. Iwapo waaminio Ukweli hawadumishwa/hawataimarishwa na imani yao katika siku hizi zenye amani, ni nini kitakachowategemeza wakati mtihani mkuu utakapokuja na amri itakapotolewa dhidi ya wale wote ambao hawataiabudu sanamu ya mnyama na kupokea chapa yake katika maisha yao; kwenye paji la uso au mikononi mwao? Kipindi hiki cha adhama hakiko mbali. Badala ya kuwa dhaifu na kutokuwa na msimamo, watu wa Mungu wanapaswa kukusanya nguvu na ujasiri kwa ajili ya wakati wa taabu.”—Ibid., pp. 250,251. [Author’s emphasis.]


Jumanne Novemba 5

3. KUJIFUNZA KUTOKA KWA ABRAHAM

a. Ni hali gani mbaya ya kiroho tunayoonywa kwa dhati? Yakobo 2:19.

“Wengi wanakubali kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu, lakini wakati huo huo wanajiweka mbali naye, na kushindwa kutubu. Dhambi zao, wanashindwa kumpokea Yesu kama Mwokozi wao binafsi. Imani yao ni kibali tu cha akili na hukumu kwa ukweli; lakini ukweli hauletwi moyoni, ili kutakasa roho na kubadilisha tabia. ”—Selected Messages, bk. 1, pp. 389, 390.

“Unaweza kuamini Ukweli wote; ila kama bado kanuni zake hazijachukuliwa katika maisha yako, ukiri wako hautakuokoa. Shetani anaamini na kutetemeka. Anatenda kazi. Anajua muda wake ni mfupi, na ameshuka chini kwa nguvu kubwa kufanya kazi zake ovu sawasawa na imani yake. Lakini watu wamkirio MUNGU hawaungi mkono imani yao kwa matendo yao. Wanaamini katika ufupi wa wakati, huku bado wanashikilia tu kwa hamu vitu vya ulimwengu huu kana kwamba ulimwengu utakaa miaka elfu kama ulivyo sasa.”—Testimonies for the Church, vol. 2, p. 161.

b. Tunawezaje kuchochewa na mfano wa Abraham? Warumi 4:1– 3; Yakobo2:20–22.

“Abraham alimwamini Mungu. Tunajuaje kwamba aliamini? Matendo yake yalishuhudia tabia ya imani yake, na imani yake ikahesibiwa kwake kuwa haki.

“Tunahitaji imani ya Abraham katika siku zetu, ili kuangaza giza linalotuzunguka, kufungia nje nuru tamu ya jua ya upendo wa Mungu, na ukuaji mdogo wa kiroho…. kila jukumu linalofanywa, kila dhabihu inayotolewa kwa jina la yesu, huleta thawabu kubwa sana. Katika tendo lenyewe la wajibu, Mungu husema na kutoa baraka zake. ”—The SDA Bible Commentary [E. G. White Comments], vol. 7, p. 936.

“Wanadamu wanahesabiwa haki kwa imani, lakini watu wanahukumiwana kupewa thawabu kulingana na matendo yao. ”— The Signs of the Times, November 20, 1884.

“Haki ya Kristo inajumuisha matendo sahihi na matendo mema kutoka katika nia safi, isiyo na ubinafsi.”—Testimonies for the Church, vol. 3, p. 528.

“Kuzishika amri za Mungu kunahitaji matendo mema kutoka kwetu, kujikana, kujitolea, na kujitoa kwa faida ya wengine, siyo kwamba kazi zetu nzuri pekee zinaweza kutuokoa, lakini hakika hatuwezi kuokolewa bila matendo mema. Baada ya kufanya yote ambayo tunaweza kufanya, basi tutasema: Hatujafanya zaidi ya wajibu wetu, sisi ni watumwa tusio na faida, tusiostahili upendeleo hata mdogo kutoka kwa Mungu. Kristo lazima awe haki yetu na taji ya furaha yetu. ”—Ibid., p. 526.


Jumatano Novemba 6

4. MANENO YA KUTIA MOYO

a. Elezea jinsi kielelezo cha maisha ya Abraham kinapaswa kuonyeshwa katika maisha yetu kama waumini katika Kristo. Mwanzo 26:5; Yakobo 2:23, 24.

“Matendo mema ni matunda ya imani. Mungu anapofanya kazi moyoni, na mwanadamu kuyakabidhi mapenzi yake kwa Mungu, na kushirikiana na Mungu, yeye anafanya katika maisha kile ambacho Mungu anafanya kazi ndani yake kwa njia ya Roho Mtakatifu, na kuna upatanisho kati ya kusudi la moyo na utendaji wa maisha. Kila dhambi lazima ikataliwe kama kitu cha chuki kilichomsulubisha Bwana wa uzima na utukufu, na muumini lazima awe na uzoefu wa maendeleo kwa kuendelea kufanya kazi za kristo. Ni kwa kuyasalimisha mapenzi daima, kwa utii wa kudumu, ndipo baraka ya kuhesabiwa haki inabaki.

“Wale wanaohesabiwa haki kwa imani lazima wawe na moyo wa kuishika njia ya Bwana. Ni ushahidi kwamba mtu hahesabiwi haki kwa imani wakati matendo yake hayalingani na mahubiri yake. Yakobo asema, ‘Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.?’ (Yakobo 2:22).

“Imani isiyozaa matendo mema haihesabii haki ya nafsi. ”—Selected Messages, bk. 1, p. 397.

b. Kwa nini wote wanaoshuhudia makafiri leo wanaweza kutiwa moyo na jinsi Rahabu, kahaba anavyotajwa kuwa ambaye Mungu alimhesabia haki? Yakobo 2:25; Waebrania 11:31.

“Katika Yeriko yenye maovu ushuhuda wa mwanamke wa kipagani ulikuwa ‘Bwana, Mungu wenu, yeye ndiye Mungu katika mbinguni juu na katika nchi chini’ Yoshua 2:11. ujuzi wa Yehova ambao ulikuwa umemjia hivyo, ulithibitisha wokovu wake….na kuongoka kwake halikuwa jambo pekee la rehema ya mungu kwa waabudu sanamu ambao walikubali mamlaka yake ya Kiungu. ”—Prophets and Kings, p. 369.

“Wote ambao, kama Rahabu, Mkanaani, na Ruthu Mmoabu waligeuka kutoka kwenye ibada ya sanamu na kuelekea kumwabudu Mungu wa kweli, walipaswa kuungana na watu wake waliochaguliwa. ”—Christ’s Object Lessons, p. 290.

“Kazi kubwa inapaswa kufanywa katika miji yetu, na mashamba yote yameiva kwa mavuno. Usikivu wetu utaitwa kila upande, kwa kuwa nafsi zilizotubu katika nchi za Kikristo na za kipagani zitapaza sauti zao kwa msaada. Kusiwe na chembe moja ya kujiinua ; usalama wako pekee ni kumtumainia Mungu. ”—The General Conference Bulletin, April 1, 1895.


Alhamisi Novemba 7

5. NJIA ZA USHINDI

a. Elezea jinsi tunavyoweza kuwa na ushindi katika kristo. Yakobo 2:26; 2 Petro 1:3, 4.

“Ni muhimu kuwa na imani katika Yesu, na kuamini umeokolewa kupitia yeye; lakini kuna hatari katika kuchukua msimamo ambao wengi huchukua katika kusema, ‘Nimeokolewa.’ Wengi wamesema: ‘Lazima mfanye matendo mema; nawe utaishi’; lakini pasipo Kristo hakuna awezaye kufanya matendo mema. Wengi katika siku hizi husema, ‘Amini, amini tu, na uishi.’ Imani na matendo huenda pamoja, kuamini na kutenda vimeunganaa. Bwana anahitaji si chini ya nafsi sasa, kama vile alivyotaka Adamu katika Paradiso kabla ya kuanguka utii mkamilifu, uadilifu usio na dosari. Hitaji la Mungu chini ya agano la neema ni pana sawa na mahitaji alifanya katika Paradiso patana na sheria yake, ambayo ni takatifu, na ya haki na njema….Mtu awaye yote asikubaliane na udanganyifu huo unaompendeza moyo wa asili, ambao Mungu ataukubali unyoofu, haijalishi imani ni ipi, hata maisha yawe yasiyokamilika kiasi gani. Mungu anataka kutoka kwake utii kamili wa mtoto.

“Ili kukidhi matakwa ya sheria, imani yetu lazima ishike haki ya Kristo, tukiikubali kuwa haki yetu. Kupitia kuungana na Kristo, kwa kukubali haki yake kwa imani sisi tunaweza kustahili kufanya kazi za Mungu, kuwa watenda kazi pamoja na kristo. Ikiwa uko tayari kupeperuka pamoja na mkondo wa uovu, na usishirikiane na mashirika ya mbinguni katika kuzuia makosa katika familia yako, na katika kanisa, ili haki ya milele iweze kuletwa, huna imani. Imani hufanya kazi kwa upendo na kutakasa roho. Kwa njia ya imani Roho mtakatifu anafanya kazi ndani ya moyo ili kuumba utakatifu ndani yake; lakini hili haliwezi kufanyika isipokuwa wakala wa kibinadamu atafanya kazi pamoja na Kristo….Ili tuwe na haki ya Kristo, tunahitaji kila siku kubadilishwa kwa uvutano wa Roho, kuwa washiriki wa asili ya Kimungu.”—Selected Messages, bk. 1, pp. 373, 374.


Ijumaa Novemba 8

MASWALI TAFAKARI BINAFSI

1. Katika kudai kushika sheria ya Mungu, ni lazima nitambue nini kuhusu ushawishi wangu?

2. Mbingu inahitaji nini kwa waumini wa kikristo?

3. Kwa nni Abraham mara nyingi anaitwa baba wa waaminifu?

4. Kati ya marafiki zangu, ni nani anayeweza kuishia kuwa Rahabu aliyeongoka?

5. Nitawezaje kuwa na uzoefu wa ushindi wa Kikristo?

 <<    >>