Jumapili
Oktoba 13
1. SABABU YA KUKUA KIROHO
a. Elezea siri jinsi Yakobo 1:2 inavyoweza kutimizwa ndani yetu. Nehemia 8:10.
“Majaribio yote yanayopokelewa kama walimu/waelimishaji yataleta furaha. Maisha yote ya kidini yatakuwa yenye kuhuisha, kuinua, kuboresha, kunukia kwa maneno na matendo mema. Adui anafurahi sana kuwa na roho zilizohuzunika, zilizoshuka, zenye kuomboleza na kuugua; anataka maoni kama hayo yatolewe kuhusu matokeo ya imani yetu. Lakini Mungu anapanga kwamba akili isichukue kiwango cha chini. Anatamani kila nafsi ipate ushindi katika uwezo wa utunzaji/kutunza wa Mkombozi. ”—Testimonies for the Church, vol. 6, pp. 365, 366.
b. Kwa nini mungu anaruhusu majaribu yaje juu yetu? Yakobo 1:3; Warumi 5:3.
“Kama tunayashinda majaribu yetu na kupata ushindi juu ya vishawishi vya shetani, ndipo tunavumilia jaribio la Imani yetu, ambayoni ya thamani kuliko dhahabu, na kuandaliwa vizuri na kuwa na nguvu kukabilina na jaribu lingine. Lakini kama tukikata tamaa na kuyapa nafasi majaribu ya shetani, tutazidi kuwa wadhaifu na hatutapata thawabu ya kujaribiwa pia hahtutakuwa tayari kukabiliana na majaribu yanayofuata. Kwa njia hii tutazidi kuwa wadhaifu zidi na Zaidi, hadi tutakuwa mateka wa vishawishi vya shetani. Tunapaswa kuvaa silaha zote za Mungu na kuwa tayari kila wakati kupambana na nguvu za giza.”— Early Writings, p. 46.
Jumatatu
Oktoba 14
2. MATOKEO BORA KULIKO TUNAVYOWAZA
a. Elezea faida za kuwa na subira. Yakobo 1:4; Luka 21:19.
“Mungu ni mwenye hekima na mwema hata kujibu maombi yetu siku zote kwa wakati na kwa jinsi tunavyotamani. Atafanya zaidi na bora zaidi kwa ajili yetu kuliko kutimiza matakwa yetu yote. Na kwa sababu tunaweza kumwamini yeye hekima na upendo, hatupaswi kumwomba akubali mapenzi yetu, lakini tunapaswa kutafuta kuingia na kutimiza kusudi lake. Matamanio yetu na maslahi yanapaswa kupotea katika mapenzi yake. Mambo haya yanayojaribu imani ni kwa manufaa yetu. Inadhirishwa ikiwa imani yetu ni ya kweli na ya dhati, kuegemea juu ya neno la mungu pekee, au iwe kutegemeana na hali, halina uhakika na linaweza kubadilika. Imani inaimarishwa na matendo. Ni lazima tuache subira ifanye kazi yake kamilifu, tukikumbuka kwamba kuna ahadi za thamani katika Maandiko kwa wale wanamngojea Bwana. ”—The Ministry of Healing, p. 231.
b. Jinsi gani na kwa nini Yakobo anatuonyesha picha kubwa kuliko mtazamo wa muda tu wa mamlaka na ustawi katika ulimwengu huu uliopotoka? Yakobo 1:9–11.
“Kwa wakati huu, kabla ya zahama ya mwisho, kabla ya uharibifu wa kwanza wa ulimwengu, watu wameingizwa katika anasa na harakati za akili. Kwa kushughulishwa na yanayooneka na ya mpito, wamepoteza dira milele. Maana vitu vinaharibika kwa kutumiwa, wanatoa dhabibu ya utajiri usioharibika. Akili zao zinahitaji kuinuliwa, maono yao ya maisha yapanuliwe. Wanahitaji kuamshwa kutoka kwa uchovu na ndoto za kilimwengu.
“Kutoka kwa kuinuka na kuanguka kwa mataifa kama yalivyowekwa wazi katika kurasa za maandiko matakatifu, wanahitaji kujifunza jinsi utukufu wa nje na wa kidunia ulivyo bure. Babeli, pamoja na nguvu zake zote na fahari yake, ambayo dunia yetu haijawahi kuiona tangu wakati huo nguvu na fahari ambayo watu wa siku hizo walionekana kuwa imara na kustahimili jinsi ambavyo imepita kabisa! Kama ‘ua la nyasi’ limeharibika hivyo huangamia yote ambayo hayana Mungu kwa msingi wake. Ni kile tu ambacho kimefungamana na kusudi lake na kudhihirisha tabia yake ndicho kinaweza kustahimili. Kanuni zake ndizo pekee ambazo zitakazoweza kudumu ulimwengu wetu unajua. ”— Education, p. 183.
“Hazina ya dunia inapita. Ni kupitia Kristo pekee ndipo tunaweza kupata utajiri wa milele. ”—The Review and Herald, December 10, 1901.
Jumanne
Oktober 15
3. KATIKA JOTO LA VITA
a. Tunapokabili majaribu, ni lazima tufanye nini kwa sala, na kwa nini? Yakobo 1:12.
“Ishini maisha ya kawaida, halisi. Iweni wakweli katika kila fikra na neno na tendo, na ”kwa unyenyekevu wa akili kila mmoja amwone mwenzake bora kuliko yeye mwenyewe.” Kumbukeni kuwa tabia ya maadili inahitaji kuboreshwa kwa kukesha na kuomba kila wakati. Mnapoendelea kumtazama Kristo, daima mko salama; lakini wakati mnapofikiria dhabihu zenu au kujitoleana shida zenu, na kuanza kujihurumia, mnapoteza tumaini lenu kwa Mungu na mnakuwa katika hatari kubwa. ”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 522.
“Tunapaswa kusonga mbele kwa kasi, bila kukata tamaa wala tumaini katika kazi njema, jaribu lolote litakalotukabili, wala giza lolote la maadili linaloweza kutuzunguka. Uvumilivu, imani, na upendo kwa wajibu ndio masomo ambayo lazima tujifunze. Kuishinda nafsi na kumtazama Yesu ni kazi ya kila siku. Bwana hataiacha kamwe nafsi inayomtegemea na kuutafuta msaada Wake. Taji ya uzima imewekwa juu ya paji la uso wa mshindi pekee. ”—Ibid., vol. 5, pp. 70, 71.
b. Kwa nini makosa kusema kwamba Mungu hutuma majaribu? Yakobo 1:13.
“Tusijaribu kupunguza hatia yetu kwa kutoa udhuru juu ya dhambi. Hatuna budi kukubali jinsi Mungu anavyoikadiria dhambi, na hilo ni jambo zito kweli. Ni Kalvari tu iwezayo kufunua ubaya mkubwa wa kutisha wa dhambi.
“Majaribu ni ushawishi wa kufanya dhambi, na huo hautoki kwa Mungu, bali unatoka kwa Shetani, na kwenye uovu uliomo mioyoni mwetu wenyewe. “Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu’ Yakobo 1:13, R.V.
“Shetani anataka kututia majaribuni, ili uovu wa tabia zetu udhihirishwe mbele ya wanadamu na mbele ya malaika, apate kudai kuwa sisi ni watu wake. Yule adui hutuongoza tufanye dhambi, ndipo hutushtaki mbele ya wale wa mbinguni kuwa hatustahili upendo wa Mungu. ”—Thoughts From the Mount of Blessing, pp. 116, 117.
c. Wakati mshitaki anaposhambulia tabia zetu zenye dosari, Bwana hututeteaje? Zakaria3:1–4; 1 Yohana 1:9–2:1.
Jumatano
Oktoba 16
4. NGUVU ZA MUNGU KATIKA UDHAIFU WETU
a. Elezea maneno katika maombi ya Bwana, “usitutie majaribuni.” ” Mathayo 6:13 (sehemu ya kwanza); Isaya 30:21.
“[Mungu] Anatuacha tupate migogoro, mateso na shida, si kama laana, bali kama mbaraka mkuu kuliko yote katika maisha yetu. Kila jaribu tunalolishinda, kila taabu tunayoivumilia, hutuletea uzoefu mpya maishani mwetu, na kutusogeza mbele katika kazi ya ujenzi wa tabia zetu. Mtu yule ambaye hushinda majaribu kwa nguvu itokayo juu, huwadhihirishia walimwengu na wote mbinguni jinsi neema ya Kristo ilivyo na nguvu.
“Lakini wakati hatupaswi kuwa na hofu kwa ajili ya taabu, japo iwe kali, tungeomba kwamba Mungu asituache twende mahali ambapo tutavutwa mbali na tamaa za mioyo yetu miovu. Katika kusali sala hiyo aliyotupa Kristo, tunajitoa wenyewe kuongozwa na Mungu, tunamwomba atuongoze katika njia zilizo salama. Hatuwezi kusali sala hii kwa moyo mnyofu, na huku tukaazimu kwenda katika njia zetu tulizozichagua wenyewe. Tutausubiri mkono wake utuongoze….
“Si salama kwetu kusitasita na kutafakari juu ya faida itakayopatikana tukiyatii mashauri ya Shetani. Dhambi humaanisha aibu na maangamizi kwa kila mtu ajifurahishaye katika hiyo; lakini kwa tabia yake inapofusha macho na kudanganya, tena inatushawishi kwa kutuletea mambo yanayovutia sana. Tukithubutu kwenda upande wa Shetani, hatuna ahadi yo yote ya kulindwa dhidi ya uwezo wake. Kwa kadiri ya uwezo ulio ndani yetu, imetupasa kufunga kila njia ambayo kwayo huyo mjaribu anaweza kupata njia ya kuingia ndani yetu.
“Sala hii, “Usitutie majaribuni,” ni ahadi kwa yenyewe. ”—Thoughts From the Mount of Blessing, pp. 117, 118.
b. Je ni ombi na uhakikisho gani ambao Mungu anatupatia kuhusu majaribu? Yakobo 1:14–16; 1 Wakorintho10:13.
“Jaribu ni nini? Ni njia ambayo wale wanaodai kuwa watoto wa mungu wanapimwa na kujaribiwa. Tunasoma kwamba Mungu alimjaribu Abraham, kwamba aliwajaribu wana wa Israeli. hii ina maana kwamba aliruhusu hali zitokee ili kujaribu imani yao na kuwaongoza kumtegemea yeye ili kupata msaada. Mungu anaruhusu majaribu yawajie watu wake leo ili watambue kuwa yeye ndiye msaidizi wao. Ikiwa wanamkaribia yeye wakati wa kujaribiwa, yeye huwatia nguvu ili kukabiliana na majaribu. ”—In Heavenly Places, p. 251.
Alhamisi
Oktoba 17
5. MAJARIBU KATIKA MTAZAMO
a. Kukaa ndani ya Kristo na kwa hivyo kukombolewa kutoka majaribuni, ni nini tunapaswa kuchagua kila wakati? Luka 4:8; Wafilipi 1:21.
“Kamwe majaribu hawezi kutulazimisha kufanya maovu. Hawezi kuongoza mawazo isipokuwa kama mawazo yamekubali kuongozwa naye. Lazima kuwepo na uhiari kwanza, lazima imani iwe imeacha kumshikilia Kristo kwanza, ndipo Shetani anaweza kututawala. Lakini kila nia ya dhambi tunayokuwa nayo inampatia Shetani mahali pa kusimama mahali petu. Kila eneo ambalo linatushinda kufikia viwango vya kimbingu ndilo mlango wake ulio wazi wa kuingilia ili kutujaribu na kutuharibu. Na kila kuanguka au kushindwa kwetu kunampatia nafasi ya kumsuta Kristo. ”—The Desire of Ages, p. 125.
b. Ni nini kinapaswa kutuchochea kusonga mbele hadi kushinda katika Kristo? Wafilipi 4:13; Ufunuo2:10 (sehemu ya mwisho); 3:21.
“Anayejazwa Roho wa Kristo hukaa ndani ya Kristo. Pigo linaloelekezwa kwake linaanguka juu ya Mwokozi, ambaye anamzunguka pande zote, akiwa pamoja naye. Lo lote limpatalo yeye linatoka kwa Kristo. Yeye hana haja ya kuupinga uovu, kwa maana Kristo ndiye mlinzi wake. Hakuna cho chote kiwezacho kumgusa isipokuwa kwa kibali chake Bwana, na “mambo yote” anayoruhusu “hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema.” Warumi 8:28.”—Thoughts From the Mount of Blessing, p. 71.
“Taji ya uzima imewekwa juu ya paji la uso wa mshindi pekee. Kuna jukumu zito kwa kila mtu la kumfanyia Mungu kazi kwa bidii wakati tukingali tunaishi. ”— Testimonies for the Church, vol. 5, p. 71.
Ijumaa
Oktoba 18
MASWALI TAFAKARI BINAFSI
1. Ninahitaji kumbuka nini wakati jaribu gumu litakaponijia?
2. Ni lazima nitambue nini kuhusu jinsi Mungu hujibu maombi?
3. Majaribu hutoka wapi, na kwa nini?
4. Nini hutokea wakati wowote tunapopinga majaribu?
5. Ninawezaje kukaa kimamilifu zaidi ndani ya kristo?