Back to top

Sabbath Bible Lessons

Masomo katika Waraka wa Yakobo

 <<    >> 
Somo la 8 Sabato, Novemba 23, 2024

Kuchagua nini cha Kufikiri

FUNGU LA KUKARIRI: “Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. ” (Mathayo 12:34, nusuya pili).

“Omba kabla ya kusema, na malaika wa mbinguni watakusaidia na watawafukuza malaika waovu, ambao wanaweza kukuongoza kutokumheshimu Mungu, kudharau kazi Yake, na kudhoofisha nafsi yako mwenyewe. ”—Testimonies for the Church, vol. 2, p. 82.

Inapendekezwa kusoma:   Thoughts From the Mount of Blessing, pp. 125-129

Jumapili Novemba 17

1. DAWA YA SUMU

a. Tunaposhambuliwa na mazoea ya usemi wa watu wenye nia mbaya, ni ujumbe gani wa Mungu kwetu, hata kati ya haya yote? Yakobo 3:7, 8; Waebrania 10:38.

“[Ndugu J] Anahurumiwa na malaika wa mbinguni, kwa maana amezungukwa na giza. Masikio yake yanasikia maneno ya kutoamini na giza kwa mfululizo. Ana mashaka na maswali yanayotupwa kila mara mbele yake. Ulimi ni ulimwengu wa uovu. “Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.” Kama Ndugu J angeshikamana na Mungu kwa uthabiti zaidi na kuhisi kwamba anapaswa kuhifadhi uaminifu na maadili yake mbele za Mungu hata kwa gharama ya uhai wake wa asili, angepokea nguvu kutoka juu. Kama anaruhusu imani yake kuathiriwa na giza na ukafiri unaomzunguka mashaka na maswali na mazungumzo mengi - hivi karibuni atakuwa kwenye giza totoro na mashaka na kutoamini, na hatakuwa na nuru wala nguvu katika Ukweli.

“Hapaswi kufikiria kwamba kwa kutafuta kuridhiana na marafiki zake, ambao wana uchungu dhidi ya imani yetu, atafanya iwe rahisi kwake. Ikiwa atasimama kwa kusudi moja la kumtii Mungu kwa gharama yoyote atapata msaada na nguvu. Mungu anampenda na kumhurumia Ndugu J. Anajua kila mashaka, kila hali ya kukatisha tamaa, kila usemi wa uchungu. Anayafahamu yote. Ikiwa ataweka kando kutokuamini kwake na kusimama katika Mungu bila kutikiswa, imani yake itaimarishwa kwa mazoezi.”—Testimonies for the Church, vol. 4, pp. 236, 237.


Jumatatu Novemba 18

2. JAMBO ZITO

a. Yale yaliyoandikwa kuhusu usemi wa udanganyifu na uchochezi na kwa nini ni lazima tuombe ili kushinda katika nyanja hii ya maisha? Zaburi 5:8–10.

“Hotuba ni mojawapo ya zawadi kuu za Mungu kwa mwanadamu. Ulimi ni kiungo kidogo, lakini maneno ambayo hutunga, yakitolewa kwa sauti yana nguvu kubwa. Bwana atangaza, ‘hakuna mtu awezaye kuufunga ulimi.’ umeweka taifa dhidi ya taifa, na umesababisha vita na umwagaji damu. Maneno yamewasha moto ambao umekuwa mgumu kuzima. Pia wameleta furaha na shangwe kwa nafsi nyingi. Na maneno yanaposemwa kwa sababu Mungu anasema, ‘sema nao maneno yangu,’ mara nyingi husababisha huzuni kwa toba.

“Kipaji cha hotuba kinabeba jukumu kubwa. Inahitaji kulinda kwa uangalifu; kwa maana ni nguvu kuu kwa uovu na kwa wema.”—The SDA Bible Commentary [E. G. White Comments], vol. 3, p. 1142.

“Lazima kuwe na matengenezo kamili katika maisha yako, mabadiliko kwa kufanywa upya nia yako. Mungu anahitaji watu Wake wakusaidie kwa sababu unahitaji msaada, na unapaswa kuwa mnyenyekevu sana ili kusaidiwa na wao. Unapojaribiwa kumwachia mshiriki mkorofi, ah! kumbuka kwamba malaika mwenye kuweka kumbukumbu anaandika kila neno. Yote yameandikwa kitabuni, na, usipooshwa kwa damu ya Kristo, lazima ukutane nayo tena. Sasa una kumbukumbu isiyo safi mbinguni. Toba ya dhati mbele za Mungu itakubaliwa. Unapokaribia kuzungumza kwa hasira na shauku, funga kinywa chako. Usiseme neno.”—Testimonies for the Church, vol. 2, p. 82.

b. Elezea jinsi maneno yetu yanavyotoka kwa wingi ya kile tunachokifikiri na kuhusu namna tulivyo. Yeremia17:9; Mathayo 12:33–37; 14:6–8.

“Maudhui ya mazungumzo hufunua hazina ya moyo. Mazungumzo yasiyo ya thamani, ya kawaida, maneno ya kubembeleza, midhaa ya kipumbavu, yanayosemwa ili kuunda kicheko, ni biashara ya shetani, na wote wanaojiingiza katika mazungumzo haya ni biashara ya bidhaa zake. Mivuto inafanywa kwa wale wanaosikia mambo haya sawa na yale yaliyofanywa na Herode wakati binti wa Herode aliyecheza mbele yake. Shughuli hizi zote zimeandikwa katika vitabu vya mbinguni; na siku kuu ya mwisho watatokea katika nuru zao za kweli mbele ya wakosefu. Ndipo wote watakapotambua ndani yao matendo ya kuvutia na ya udanganyifu ya ibilisi, ili kuwaongoza kwenye njia pana lango pana linalofungua kwa uharibifu wao. ”—Testimonies to Ministers, pp. 84, 85.


Jumanne Novemba 19

3. MOYO WOTE UNAHITAJIKA

a. kwa nini tutegemee usemi thabiti kutoka kwa waumini katika ukweli uliopo? Yakobo 3:9, 10. Ni onyo gani linalotolewa ikiwa tunashindwa kuhusu jambo hili.

“Ikiwa mtakuwa na mazoea ya kuthamini hisia kwamba Mungu huona na kusikia yote unayofanya na kusema, na kuweka kumbukumbu ya uaminifu ya maneno na matendo yenu yote, na kwamba lazima mkutane nayo yote, basi katika yote mnayofanya na kusema mtatafuta kufuata maagizo ya dhamiri iliyoelimika na kuamka. Ulimi wenu utatumiwa kwa utukufu wa Mungu na utakuwa chanzo cha baraka kwenu na kwa wengine. Lakini kama mkijitenga na Mungu kama mnavyofanya, jihadharini usije ulimi wenu ukadhihirisha ulimwengu wa uovu na kukuleteeni hukumu ya kutisha; kwa kuwa roho zitapotea kupitia ninyi/kwenu.”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 244.

b. Ni sala gani inaweza kutusaidia kufikiri na kuzungumza kwa uthabiti zaidi? Zaburi 86:11.

“Ikiwa mpokeaji wa maarifa ya Biblia hafanyi mabadiliko yoyote katika mazoea au matendo yake kuendana na nuru ya kweli, nini basi? je! Roho anapigana vita na mwili, na mwili dhidi ya roho; na mmoja wa hawa lazima ashinde. Ikiwa kweli huitakasa nafsi, dhambi inachukiwa na kuepukwa, kwa sabababu kristo anakubaliwa kuwa mgeni mwenye kuheshimiwa. Lakini kristo hawezi kushiriki moyo uliogawanyika; dhambi na yesu kamwe hawako katika ushirika. ”—Testimonies to Ministers, p. 160.

“Kesha na uombe daima. Jitoe nafsi yako kikamilifu kwa Bwana na haitakuwa vigumu kumtumikia. Una moyo uliogawanyika. Hii ndio sababu giza badala ya nuru linakuzingira. Ujumbe wa mwisho wa rehema sasa unatolewa. Ni ishara ya uvumilivu na huruma ya Mungu. Njoo! Ndiyo mwaliko unaotolewa sasa. Njooni! kwa maana vitu vyote viko tayari sasa. Huu ni mwito wa mwisho wa rehema. Baadae kitakuja kisasi cha Mungu Mwenye ghadhabu. ”—Testimonies for the Church, vol. 2, p. 225.

“Ni kwa moyo wote, ni wanaume na wanawake walioamua kwa moyo wote, ndio watakaosimama sasa. Kristo aliwapepeta wafuasi Wake tena na tena, hadi wakati fulani walibaki kumi na mmoja na wanawake wachache waaminifu walioweka msingi wa kanisa la Kikristo. Wapo wale ambao watasimama nyuma wakati mzigo unapaswa kubebwa; lakini wakati kanisa linapowaka na kung’aa, wanapata shauku, wanaimba na kupiga kelele, na kusisimka; lakini kuweni makini nao. Shauku inapokwisha, ni akina Kalebu wachache tu waaminifu watakaokuja mbele na kuonesha kanuni isiyotetereka. Hawa ni chumvi ambayo huhifadhi harufu. ”—Ibid., vol. 5, p. 130.


Jumatano Novemba 20

4. MAJI KUTOKA KWENYE CHEMCHEM SAFI

a. Ni kanuni gani inayofunua kwamba moyo pekee uliofanywa upya kwa neema ya Mungu unaweza kuleta matendo thabiti? Yakobo 3:11, 12. toa mifano fulani inayofaa.

“Unadhifu na utaratibu wa mavazi, na usafi katika makao yote, vinapaswa kuzingatiwa kwa uthabiti na watunza-sabato, ambao wanaonekana kuwa wa ajabu, na wanaangaliwa kwa ajili ya makosa yao. Ushawishi wao unapaswa kuwa mtakatifu. Kweli takatifu ambazo tunakiri kamwe hazitawashushia hadhi wapokezi, na kuwafanya wawe wakali na wakorofi, wasiojali nafsi zao, na wachafu katika nyumba zao. Ikiwa mpokezi ana tabia ya ulegevu, ukweli humwinua, na kumfanyia matengenezo kamili. Isipokuwa ukweli una athari hii, mtu binafsi hajahisi uwezo wake wa kuokoa. Kutojari na mavazi yasiyo na utaratibu sio alama ya unyenyekevu. Hapa wengine wamejidanganya. Maisha, matendo, maneno, yatasema ikiwa mtu huyo ana unyenyekevu wa kweli, na mavazi hayo yataambatana na matunda yaliyodhihirishwa. Chemchemi safi haiwezi kutoa maji matamu na machungu. Safisha chemchemi na vijito vitakuwa safi. Nyumba ya Mungu mara nyingi hunajisiwa na watoto wa watunza-sabato. Wazazi wao huwaruhusu kukimbia kuzunguka nyumba, kucheza, kuzungumza, usikivu wa watu, na wadhihirishe hasira zao mbaya katika mikutano ile ile ambapo wamekusanyika ili kumwabudu Mungu. Nimeona kwamba katika kusanyiko la watakatifu utulivu mtakatifu utawale. Lakini nyumba ambamo watu wa Mungu hukusanyika mara nyingi hufanywa kuwa Babeli kamilifu, mahali pa fujo. Hii haimpendezi Mungu. Ikiwa wazazi hawana udhibiti, na hawawezi kuwadhibiti watoto wao katika mkutano, Mungu angependezwa zaidi kubaki nao nyumbani na watoto wao wakorofi. Afadhali wapate hasara ya mikutano, kuliko kuwa na idadi kubwa ya kuudhi, na mikutano yao kuharibika. Wazazi wakiwaacha watoto wao bila kudhibitiwa, bila kutiishwa nyumbani. Hawawezi kuwaruhusu wafanye wapendavyo katika mikutano. Nani anapaswa kuwajibika katika jambo hili? Hakika ni wazazi, awapaswi Kuhisi taabu ikiwa wengine hawataki amani yao ivurugike wanapokutana ili kumwabudu Mungu.

“Wazazi ndi wanapaswa kuwajibika katika jambo hili, na huenda likawapelekea kuona na kutimiza wajibu wenu uliopuuzwa. mkiwabeba watoto wenu hadi kwenye nyumba ya Mungu wanapaswa kueleweshwa kwamba wao ni mahali ambapo Mungu hukutana na watu wake. Hakuna utaratibu ule unaozingatiwa kati ya watunza -sabato katika suala hili ambapo upo katika makanisa ya jina. Wazazi, mnakazi ya kufanya. Kuwatiisha watoto wenu nyumbani, nawe unaweza kuwatawala katika nyumba ya Mungu.”— Spiritual Gifts, vol. 2, pp. 288, 289.


Alhamisi Novemba 21

5. HEKIMA NA KUPEWA MAARIFA

a. Kwa nini kila mmoja wetu anahitaji kuchunguza mtazamo wake kutoka ndani kwenda nje -moyoni, neno, na tendo? 2 Wakorintho 13:5.

“ ‘Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe . (2 Wakorintho 13:5). kosoa hasirakwa ukaribu, tabia, mawazo, maneno, mielekeo,makusudi, na matendo. Tunawezaje kuomba kwa akili mambo tunayohitaji isipokuwa tuthibitishe kwa maandiko hali ya afya afya yetu ya kiroho?”—Selected Messages, bk. 1, p. 89.

“Ndugu na dada zangu, mnatumia vipi zawadi ya usemi? Je! mmejifunzakudhibiti ulimi ili uweze kutii maagizo ya dhamiri iliyoangaziwa na mapenzi matakatifu? Je! Mazungumzo yenu hayana mizaha, kiburi na uovu, udanganyifu na uchafu? Je! hamna hila mbele za Mungu? Maneno yana nguvu kubwa. Shetani kama ikiwezekana ataufanya ulimi uwe hai katika huduma yake. Kwa sisi wenyewe hatuwezi kumdhibiti mshiriki asiye na nidhamu wa mwili wetu, yaani ulimu. Ni neema ya Bwana ndiyo tumaini letu pekee.”—Testimonies for the Church, vol. 5, p. 175.

“Yeye anayejiweka mwenyewe bila kujibakiza chini ya uongozi wa Roho wa Mungu, atapata kwamba akili yake inapanuka na kukua. Anapata elimu katika hudumu ya Mungu isiyoegemea upande mmoja na yenye upungufu, inayokuza tabia ya upande mmoja, bali yenye matokeo ya ulinganifu na ukamilifu. Udhaifu ambao umedhihirika katika utashi unaoyumba na tabia isiyo n nguvu, unashindwa, kwa maana ibada na uchaji Mungu humleta mtu huyo katika uhusiano wa karibu sana na Kristo. Yeye ni mmoja na Kristo, mwenye utimamu na nguvu za kanuni. Ufahamu wake uko wazi, naye hudhihirisha hekima hiyo inayotoka kwa Mungu. ”—Selected Messages, bk. 1, p. 338.


Ijumaa Novemba 22

MASWALI TAFAKARI BINAFSI

1. Nijibuje ninapokabiliwa na mazungumzo yenye sumu?

2. Watu wanaposema mambo ,inaashiria nini hasa kuwahusu?

3. Elezea vita vinavyoendelea katika akili ya mwanadamu, na jinsi ambavyo vinaweza kushinda.

4. Ni tabia /mielekeo gani ya mgodi ambayo inaweza kuwa inaonyesha maji machafu ndani?

5. Jinsi gani na kwa nini namna yangu ya kuzungumza ibadilishwe?

 <<    >>