Back to top

Sabbath Bible Lessons

Masomo katika Waraka wa Yakobo

 <<    >> 
Somo la 10 Sabato, Desemba 7, 2024

Kushinda Mtazamo wetu wa Matatizo

FUNGU LA KUKARIRI: “Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbilia. ” (Yakobo 4:7).

“Upendo kwa Ukweli safi, uliotakaswa, upendo kwa Mkombozi Mpendwa, itarahisisha kazi ya kushinda.”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 38.

Inapendekezwa kusoma:   Testimonies for the Church, vol. 3, pp. 39-47

Jumapili Desemba 1

1. HAKI ISIYO NA UBINAFSI

a. Taja sifa mbili za mwisho zilizotajwa katika orodha ya hekima iliyozaliwa Mbinguni. Yakobo 3:17 (sehemu ya mwisho).

“Mtume Yuda anasema: “Wahurumieni wengine walio na shaka.” Tofauti hii si ya kutekelezwa katika roho ya upendeleo. Hakuna uso unaopaswa kuoneshwa roho inayodokeza: “Ikiwa utanipa upendeleo, nami nitakupendelea.” Hii ni sera isiyotakaswa, ya kidunia, na ambayo haimpendezi Mungu. Ni kulipa fadhila na pongezi kwa ajili ya kupata faida. Inaonesha upendeleo kwa baadhi ya watu, wakitarajia kupata manufaa kupitia kwao. Ni kutafuta nia yao njema kwa kujiridhisha binafsi au kujiendekeza mwenyewe, ili tuheshimiwe kwa makadirio makubwa zaidi ya wengine kwamba tunastahili kama sisi wenyewe.”—Testimonies for the Church, vol. 4, pp. 221, 222.

“Mungu hapendezwi na kazi ya uvivu inayofanywa katika makanisa. Anatarajia mawakili wake wawe wa kweli na waaminifu katika kutoa karipio na kusahihisha. Wanapaswa kufukuza makosa kwa kanuni ambayo Mungu ametoa katika Neno Lake, si kulingana na mawazo na misukumo yao wenyewe. Isiwepo hali ya ukali kutumika, wala kuto kuwa na haki, uharaka, na kazi za msukumo kufanyika. Juhudi zinazofanywa kulisafisha kanisa kutokana na uchafu wa kiadili lazima zifanywe kwa njia ya Mungu. Kusiwe na upendeleo, hakuna unafiki. Ni lazima pasiwepo na watu wapendao, ambao dhambi zao zinachukuliwa kuwa ni dhambi kidogo kuliko za wengine. Loo, ni kiasi gani sisi sote tunahitaji ubatizo wa Roho Mtakatifu. Kisha tutafanya kazi daima na nia ya Kristo, kwa wema, huruma, na faraja, tukionyesha upendo kwa mtenda dhambi huku tukichukia dhambi kwa chuki kamilifu.”—The Ellen G. White 1888 Materials, p. 144.


Jumatatu Desemba 2

2. KUMWAKILISHA KRISTO KWA HAKI

a. Ni kwa jinsi gani Kristo anaweza tu kuwakilishwa ipasavyo katika usemi wetu? Yakobo 3:18.

“Inawezekana kwa midomo yetu tunamkiri Kristo lakini katika matendo yetu tunamkana. Matunda ya Roho yaliyooneshwa maishani ndiyo yanayoonesha kama tumemkiri. Ikiwa tumeacha yote kwa ajili ya Kristo, maisha yetu yatakuwa ya unyenyekevu, mazungumzo yetu yatakuwa ya kimbingu, na mwenendo wetu utakuwa usio na lawama. Ushawishi wenye nguvu, utakaso wa ukweli katika nafsi, na tabia ya Kristo iliyooneshwa katika maisha, huko ndiko kumkiri Yesu. Ikiwa maneno ya uzima wa milele yamepandwa mioyoni mwetu, matunda yatakuwa nihaki na amani. Tunaweza kumkana Kristo maishani mwetu kwa kupenda raha au kujipenda wenyewe, kwa mzaha na kwa utani, na kwa kutafuta heshima ya ulimwengu. Tunaweza kumkana katika sura yetu ya nje kwa kufanana na ulimwengu, kwa sura ya kiburi au mavazi ya ya gharama. Ni kwa kukesha tu kila wakati na kuvumilia kwa maombi yasiyokoma ndipo tunapoweza kuonesha katika maisha yetu tabia ya Kristo au ushawishi wa ukweli unaotakasa.Wengi humfukuza Kristo kutoka kwenye familia zao kutokana na roho ya papara na shauku. Watu wa aina hiyo wana kitu cha kushinda katika jambo hili.”—Testimonies for the Church, vol. 1, pp. 303, 304.

b. Ni mielekeo gani ya kawaida ya kibinadamu ambayo hujitokeza katika maisha ya kila siku ambayo kwa kweli inahitaji kukomeshwa—na kwa nini? Yakobo 4:1–3.

“Ni jambo la kusikitisha kutoridhika na mazingira yetu au mazingira ambayo tumewekwa ambapo majukumu yetu yanaonekana kuwa ya unyenyekevu na yasiyo na umuhimu. Wajibu wa kibinafsi na unyenyekevu hayakufurahishi huna pumziko, huna raha, huna kuridhika. Yote haya yanatokana na ubinafsi….

“Wale ambao wanaojiita Wakristo ambao daima hunung’unika na kulalamika, na huonekana kufikiria kwamba furaha na uso wa ucheshi ni dhambi, hawana vazi la Kweli la dini.”—Ibid., vol. 3, p. 334.

“Je, nile kiasi maradufu mara kwa mara, kwa sababu ina ladha nzuri, ningewezaje kuinama na kumuomba mungu anisaidie katika kazi yangu ya uandishi, wakati sikuweza kupata wazo kwa sababu ya ulafi wangu? Je, ninaweza kumwomba mungu atunze mzigo huo usio na akili juu ya tumbo langu? Huko kungekuwa ni kumvunjia heshima. Hiyo itakuwa ni kuuliza kula juu ya tamaa yangu. Sasa ninakula kile ninachofikiri ni sawa, na kisha ninaweza kumwomba anipe nguvu ya kufanya kazi ambayo amenipa kufanya. ”—Ibid., pp. 373, 374.

“ Wakati dini ya Kristo inatawala moyoni, dhamiri inakubali, na amani na furaha vinatawala; Shida na mtanziko vinaweza kuzunguka, lakini kuna nuru katika nafsi.”—Ibid., vol. 4, p. 47.


Jumanne Desemba 3

3. KUEPUKA MITEGO YA KAWAIDA

a. Ni kanuni gani kuu iliyo muhimu katika uhusiano halisi na Kristo, tofauti na imani ya juujuu tu katika jina pekee? Yakobo 4:4.

“Wale wanaoanza maisha yao ya Kikristo kwa nusu nusu, hatimaye watapatikana wakiwa wameorodheshwa kwenye upande wa adui, chochote ambacho huenda kilikuwa nia yao ya kwanza. Na kuwa muasi, msaliti kwa njia ya Mwenyezi Mungu, ni mbaya zaidi kuliko kifo; maana yake ni upotevu wa uzima wa milele.

“Wanaume na wanawake wenye nia mbili ni washirika bora wa Shetani. Maoni yoyote mazuri wanayoweza kuwa nayo juu yao wenyewe, wao ni wapotoshaji. Wote walio washikamanifu kwa Mungu na kweli wanapaswa kusimama imara kwa ajili ya yaliyo sawa kwa sababu ni sawa. Kufunga nira pamoja na wale ambao hawajawekwa wakfu, na bado kuwa waaminifu kwa ukweli, ni jambo lisilowezekana. Hatuwezi kuungana na wale wanaojitumikia wenyewe, wanaofanya kazi katika mipango ya kidunia, na tusipoteze uhusiano wetu na Mshauri wa mbinguni. Tunaweza kujiokoa kutoka kwa mtego wa adui, lakini tumechubuliwa na kujeruhiwa, na uzoefu wetu ni mdogo.”—The Review and Herald, April 19, 1898.

b. Kwa nini ni lazima tung’oe kwa uthabiti kila mwelekeo mmoja wa wivu? Yakobo 4:5, 6 .

“Kasoro moja kubwa katika tabia ya Sauli ilikuwa kupenda kwake sifa. Sifa hii ilikuwa na ushawishi unaotawala juu ya matendo na mawazo yake; kila kitu kilionyeshwa na hamu yake ya kusifiwa na kujiinua. Kiwango chake cha mema na mabaya kilikuwa kiwango cha chini cha makofi maarufu. Hakuna mtu aliye salama aishiye ili awapendeze watu, wala hatafuti ukubali wa Mungu kwanza.”— Patriarchs and Prophets, p. 650.

“Ni wivu uliomfanya Sauli ahuzunike na kumweka hatarini mtu mnyenyekevu wa kiti chake cha enzi. Je, tabia hii mbaya ya imetenda uovu gani katika ulimwengu wetu! Uadui uleule ulikuwepo ndani ya moyo wa Sauli ambao ulichochea moyo wa Kaini dhidi ya ndugu yake Abeli, kwa sababu matendo ya Abeli yalikuwa ya haki, na Mungu alimheshimu, na matendo yake mwenyewe yalikuwa maovu, na Bwana hangeweza kumbariki. Wivu ni uzao wa kiburi, na ukiwekwa moyoni, utasababisha chuki, na hatimaye kulipiza kisasi na kuua.”—Ibid., p. 651.

“Utii, upendo, na shukrani kwa Mungu huweka mwanga wa jua moyoni, ingawa siku inaweza kuwa na mawingu mengi. Kujikana mwenyewe na msalaba wa Kristo uko mbele yako. Je! Utainua msalaba?”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 47.


Jumatano Desemba 4

4. KUZINGATIA NA KUJITOA

a. Ni jambo gani muhimu hutupatia ushindi wa kweli na wa kudumu katika Kristo? Yakobo 4:7.

“Wengine wanahisi hitaji lao la upatanisho, na kwa kulitambua hitaji hili, na shauku ya mabadiliko ya moyo, mapambano huanza. Kukataa mapenzi yao wenyewe, labda vitu vyao walivyochagua kuvipenda au kuvitafuta, inahitaji juhudi, ambayo wengi husita na kuyumba na kurudi nyuma. Walakini vita hii lazima ipigwe na kila moyo ambao umeongoka Kweli. Lazima tupigane na vishawishi nje na ndani. Lazima tupate ushindi juu ya ubinafsi, tusulubishe mapenzi na tamaa; na kisha tuanze umoja wa roho na Kristo. Kama tawi kavu na lisilo na uhai likiwa limepandikizwa kwenye mti ulio hai, ndivyo tunavyoweza kuwa matawi hai ya Mzabibu wa Kweli. Na matunda yaliyozaliwa na Kristo yatazaliwa na wafuasi Wake wote. Baada ya umoja huu kuundwa, unaweza kuhifadhiwa tu kwa kuendeleza bidii za dhati na juhudi. Kristo hutumia nguvu Zake kuhifadhi na kulinda muunganiko huu mtakatifu, na mwenye dhambi tegemezi, asiyeweza kujisaidia lazima afanye sehemu yake kwa nguvu isiyochoka, vinginevyo shetani kwa nguvu yake ya kikatili, ya hila atamtenga mtu huyo na Kristo.

“Kila Mkristo lazima ajilinde kila wakati, akiangalia kila njia ya moyo/roho ambayo shetani anaweza kuitumia kumfikia. Lazima aombe msaada wa Mungu na wakati huo huo kwa uhakika kabisa aupinge kila mwelekeo wa kutenda dhambi. Kwa ujasiri, kwa imani, kwa bidii isiyochoka, anaweza kushinda. Lakini akumbuke kwamba ili kupata ushindi Kristo lazima akae ndani Yake na yeye ndani ya Kristo.”—Testimonies for the Church, vol. 5, p. 47.

b. Paulo anarudiaje maelezo ya Yakobo kuhusu uhai wa kiroho katika maisha ya Kikristo? Warumi 6:6–11.

“Mawazo ya ulimwengu, ubinafsi, na tamaa vimekuwa vikitafuna hali ya kiroho na maisha ya watu wa Mungu. ”—Ibid., vol. 1, p. 141.

“Tunahitaji imani thabiti zaidi na ibada yenye bidii zaidi. Tunahitaji kufa nafsi zetu, na katika akili na moyo kuthamini upendo wa kuabudu kwa Mwokozi wetu. Tutakapomtafuta Bwana kwa moyo wote tutampata, na mioyo yetu yote itawaka kwa upendo Wake. Nafsi itazama katika kutokuwa na umuhimu, na Yesu atakuwa yote na katika yote kwa nafsi. . . . .

“Ni lazima tumkaribie Mungu. Ni lazima tuwe watenda kazi pamoja Naye, vinginevyo udhaifu na makosa yataonekana katika yote tunayofanya. ”— Ibid., vol. 6, p. 51.


Alhamisi Desemba 5

5. TAFAKARI KWA MAOMBI YA KIASI

a. Ni uhakikisho gani na mwito gani wa kutafakari kila mmoja wetu katika vita dhidi ya mielekeo yetu wenyewe miovu? Wakolosai 3:1–3; Yakobo 4:8, 9 .

“Haiwezekani kwa yeyote kuutambua ukweli wakati ulimwengu umeyachukua mapenzi yao. Ulimwengu unaingilia kati yao na Mungu, ukificha maono na kupunguza hisia kwa kiwango kwamba hawawezi kuvitambua vitu vitakatifu. Mungu huwaita watu kama hawa: „Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.” Wale ambao wameichafua mikono yao kwa uchafu wa ulimwengu wanatakiwa kujisafisha kutokana na madoa yake. Wale ambao wanafikiri wanaweza kuutumikia ulimwengu wakiwa wanampenda Mungu wana nia-mbili. Hawawezi kumtumikia Mungu na mali. Ni watu wenye nia mbili, wanaupenda ulimwengu na wanapoteza hisia zote za wajibu wao kwa Mungu, na bado wanakiri kuwa ni wafuasi wa Kristo. Wao hawako kwa hiki wala kile. Wataupoteza ulimwengu wote endapo hawataitakasa mikono yao na kusafisha mioyo yao kwa kutii kanuni safi za ukweli. ”—Testimonies for the Church, vol. 1, pp. 530, 531.

b. Ni nini kinatokea tunaposujudu mbele za Mungu kwa unyenyekevu? Zaburi 34:18; 1 Petro 5:6, 7 .

“Ikiwa sasa utanyenyekea mbele za Mungu, na kuungama makosa yako, na kumrudia kwa moyo wako wote, unaweza kuwa bado familia yenye furaha. Kama hautafanya hivi, lakini ukaishia kuchagua njia yako mwenyewe, furaha yako ipo ukingoni. ”—Ibid., vol. 2, p. 304.


Ijumaa Desemba 6

MASWALI TAFAKARI BINAFSI

1. Nikichunguza kwa kina nia yangu ya ndani, ni katika maeneo gani ninaweza kuwa mnafiki?

2. Taja baadhi ya njia ambazo kwazo maneno yetu mara nyingi humwakilisha Kristo vibaya.

3. Ni katika maana gani wivu ni kukana imani kwa uzito—na kumtukana Mungu?

4. Kwa nini nahitaji kuwa mfu kwa nafsi yangu ili niwe hai katika Kristo?

5. Je, somo hili lina muhtasari gani baadhi ya masuala ya kweli ninayohitaji kushinda?

 <<    >>