Jumapili
Oktoba 20
1. MTOAJI MKAMILIFU
a. Ni nini kinachodhihirisha wema mkuu wa Mungu kwetu? Yakobo 1:17.
“Upendo wa Kristo kwa watoto wake ni wa dhati na ulio na nguvu. Na hivyo una nguvu kuliko kifo; kwa maana alikufa ili kuununua wokovu wetu, na kutufanya wamoja naye, kwa fumbo la milele. Upendo wake una nguvu sana kwamba unatawala nguvu zake zote, na hutumia rasilimali nyingi za mbinguni katika kuwatendea watu wake mema. Haina kubadilika-badilika au kivuli cha kugeuka ndiye yule jana, leo, na hata milele. Ingawa dhambi imekuwepo kwa muda mrefu, ikijaribu kupinga upendo huu na kuzuia utiririko wake wa ardhi, bado inatiririka kwa wingi kwa wale ambao Kristo aliwafia.
“Mungu anawapenda malaika wasio na dhambi, wanaofanya huduma yake na ni watiifu kwa amri zake zote; lakini hawapi neema; hawajawahi kuhitaji, kwa maana hawajawahi kufanya dhambi. Neema ni sifa iliyoonyeshwa kwa wanadamu wasiostahili. Hatukuitafuta; ilitumwa kututafuta. Mungu anafurahi kuwapa neema wale wote wenye njaa na kiu kwa ajili yake, si kwa sababu sisi tunastahili, bali kwa sababu hatustahili. Hitaji letu ni ustahili unaotupa uhakikisho wa kwamba tutapokea zawadi. —Testimonies to Ministers, p. 519.
b. Jinsi gani na kwa nini tumezaliwa na mungu? Yakobo 1:18; 1 Peter 1:23; 2:9.
Jumatatu
Oktoba 21
2. KUPOZA JOTO
a. Katika ulimwengu wa hasira, ni kwa jinsi gani na kwa nini tunapaswa kuwa tofauti? Yakobo 1:19.
“Iweke sheria ya kutozungumza neno la kukemea kila mmoja, bali pongeza na kusifu kila unapoweza.
“Wengine hudhani kuwa ni fadhila/wema usiopaswa kuzuiliwa, nao wataongea wakiisifia tabia yao ya kusema waziwazi ya kuongea mambo yasiyokubalika yaliyo moyoni. Wanaacha roho ya hasira ijichoshe katika mkondo wa shutuma na kutafuta-laumu. Kadri wanavyozungumza, ndivyo wanavyozidi kusisimka, na Shetani husimama karibu kusaidia kazi hiyo, kwa kuwa inamfaa. Maneno hayo yanamkasirisha yule anayeambiwa, nayo yaweza kujirudia, na kutoa uchochezi kwa maneno makali zaidi, mpaka jambo dogo limewasha moto mkubwa. Nyote wawili mnahisi kwamba mna majaribu yote ambayo mnaweza kustahimili na kwamba maisha yenu hayana furaha zaidi. Anzeni kwa dhati kazi ya kudhibiti mawazo yenu, maneno yenu, na matendo yenu. Wakati mmoja wenu anahisi kuongezeka kwa chuki, wekeni sheria ya kwenda peke yenu na kuomba kwa unyenyekevu kwa Mungu.”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 243.
b. Kwa nini hasira kali haimpendezi Mungu na inatibiwaje? Yakobo 1:20.
“Wengine wana woga, na wakianza kushindwa kujizuia katika neno au roho chini ya uchochezi, wanalewa sana na ghadhabu. Kama vile mlevi anavyotumia vileo . hawatafakari, na si rahisi kushawishiwa au kusadikishwa. Hawana akili timamu; shetani kwa wakati huu ana udhibiti kamili. Kila moja ya maonyesho haya ya hasira hudhaifisha mfumo wa fahamu na nguvu za kimaadili, na inafanya kuwa vigumu kuzuia hasira katika uchochezi mwingine.
“Pamoja na darasa hili kuna dawa moja tu kujidhibiti vizuri chini ya hali zote. Jitihada za kuingia mahali pazuri, ambapo ubinafsi hautaudhika, unaweza kufanikiwa kwa muda; lakini shetani anajua mahali pa kupata roho hizi maskini, na atazishambulua katika udhaifu wao tena na tena. Watakuwa na wasiwasi daima mradi tu wanajifikiria sana….Lakini kuna tumaini kwao. Wacha maisha haya yawe na dhoruba sana migogoro na wasiwasi, kuletwa katika uhusiano na kristo, na kisha nafsi haidai kwa ajili ya ukuu….Wanapaswa kujinyenyekeza wakisema waziwazi, ‘Nimefanya kosa. Je, utanisamehe? Kwa maana Mungu amesema tusiache jua litue juu ya ghadhabu yetu,’hii ndiyo njia pekee iliyo salama kuelekea kushinda.”—Sons and Daughters of God, p. 142.
Jumanne
Oktoba 22
3. KUTUNZA NURU
a. Elezea wito wa Mungu kwa kila mmoja wetu. Yakobo 1:21.
“Ee, ni jinsi gani yeyote aliye na nuru ya ukweli, nuru kuu waliyopewa na Mungu, anaweza kukataa ghadhabu na hukumu za Mungu kwa kumtenda dhambi na kufanya mambo yale yale ambayo Mungu amewaambia katika Neno lake kutokufanya? Wanawezaje kupofushwa na shetani kiasi cha kumvunjia Mungu heshima mbele ya uso wake, na kuzitia unajisi nafsi zao kwa kufanya dhambi wakijua? Asema mtume, ‘tumefanywa kuwa tamasha kwa ulimwengu, na kwa malaika, na kwa wanadamu.’ Je! Hawa wenye dhambi nitawaita wanafiki? Katika Sayuni uliza, Ni kwa namna gani mimi ni tamasha kwa ulimwengu, na kwa malaika, na kwa wanadamu? Jijibuni wenyewe, Kwa matumizi mabaya yangu ya nuru na mapendeleo na rehema alizo nazo mungu alinipa, kwa matendo machafu ambayo yanaharibu na kuchafua roho. ”—Testimonies to Ministers, p. 447.
b. Neno la Mungu linahusiana vipi na wokovu wetu, hasa katika siku za mwisho? 2 Timotheo 3:15; 1 Wakorintho15:1, 2.
“Kazi ya kweli ya Roho Mtakatifu juu ya mioyo ya wanadamu imeahidiwa, ili kutoa ufanisi kupitia Neno. Kristo ametangaza Neno kuwa roho na uzima….
“Shetani atafanya kazi kwa njia ya hila zaidi kutambulisha uvumbuzi wa wanadamu waliovikwa mavazi ya malaika lakini nuru itokayo katika Neno inaangaza katikati ya giza la maadili; na Biblia haitaondolewa kamwe na maonyesho ya kimuujiza. Ukweli lazima uchunguzwe, lazima utafutwe kama hazina iliyofichwa. Nuru za ajabu hazitatolewa kando na Neno, ama kuchukua mahali pake. Shikamana na Neno, lipokee Neno lilopandikizwa, ambalo litawahekimisha wanadamu hata kupata wokovu. ”—Selected Messages, bk. 2, p. 100.
“Wale wanaoikumbatia Kweli wanapaswa kutafuta ufahamu wa Kweli wa maandiko na ufahamu halisia kimatendo wa Mwokozi aliye hai. Akili inapaswa kukuzwa, na kumbukumbu kushughulishwa. Uvivu wote wa kiakili ni dhambi, na uchovu wa kiroho ni kifo.”—Testimonies for the Church, vol. 4, p. 399.
“Wakati maneno yake ya maagizo yamepokelewa, na kutumiliki, kwetu Yesu ni uwepo wa kudumu, anayetawala mawazo na matendo yetu. Tumejazwa na maagizo ya mwalimu mkuu aliyewahi kujua ulimwengu. ”—Messages to Young People, p. 160.
Jumatano
Oktoba 23
4. KIOO CHA SHERIA YA MUNGU
a. Kwa nini ni muhimu tuchunguze mioyo yetu? Yakobo 1:22–24.
“Wengi hupokea sifa kwa wema ambao hawana. Mchunguzi wa mioyo hupima nia, na mara nyingi hufanya kazi ya kupongeza sana yanayoongozwa na wanadamu yameandikwa naye kama yanayotokana na ubinafsi na unafiki duni. Kila tendo la maisha yetu, liwe zuri na la kusifiwa, au la kustahili kulaaniwa, huhukumiwa na mchunguzi wa mioyo kulingana na nia iliyomsukuma.
“Wengi hupuuza kujiangalia kwenye kioo kinachodhihirisha kasoro za tabia; kwa hivyo udhaifu na dhambi zinadumu, na ni dhahiri kwa wengine, ikiwa hazieleweki na wale walio na makosa. Dhambi ya chuki ya ubinafsi ipo kwa kiwango kikubwa, hata kwa wengine wanaodai kujitoa kwa kazi ya mungu. Ikiwa wangelinganisha tabia zao na matakwa yake, hasa na kiwango kikuu cha sheria ya mungu takatifu, wangehakikisha, kama wachunguzi wa bidii, waaminifu, kwamba kwa uwoga wamepungukiwa. Lakini wengine hawako tayari kutazama mbali vya kutosha au ndani vya kutosha kuona upotovu wa mioyo yao wenyewe. Wanataka katika mambo mengi sana, lakini wanabaki katika kutojua hatia yao kwa hiari. ”—Gospel Workers, pp. 275, 276.
b. Elezea uzuri wa uhuru wa kweli kupitia nguvu ya uumbaji inayokuja kwa kujisalimisha kwa kristo na mapenzi yake. Yakobo1:25; Yohana 8:32.
“Katika kazi ya ukombozi hakuna kulazimisha kwa nguvu. Hakuna nguvu ya nje inayotumika. Chini ya ushawishi wa Roho wa Mungu, mwanadamu huachwa huru kuchagua nani wa kumtumikia. Katika badiliko linalotokea wakati mtu anapojisalimisha kwa Kristo, kuna kiwango cha juu kabisa cha uhuru. Kuilazimisha dhambi ni tendo la moyo wenyewe. Kweli, hatuna nguvu ya kutuwezesha kutoka katika utawala wa Shetani; lakini tunapoamua kuwa huru mbali na dhambi, na katika uhitaji mkubwa tukalilia nguvu iliyo nje na juu yetu wenyewe, nguvu za moyo zinajazwa na nguvu ya mbinguni ya Roho Mtakatifu, na zinatii maongozi ya matakwa ya kutimiza mapenzi ya Mungu.
“Hali pekee ambayo uhuru wa mwanadamu unawezekana ni ile ya kuwa kitu kimoja na Kristo. ”Kweli itawaweka huru” na Kristo ndiye kweli. Dhambi inaweza kushinda tu kwa njia ya kudhoofisha akili, na kuharibu uhuru wa moyo. Kutiishwa kwa Mungu ni njia ya mtu kurejeshwa, - kwenda katika utukufu na heshima ya kweli ya mtu. Sheria ya kimbingu, ambayo tumetiishwa kwayo, ni ”sheria ya uhuru.” Yakobo 2:12. ”—The Desire of Ages, p. 466.
Alhamisi
Oktoba 24
5. DINI YA KWELI
a. Taja kipengere muhimu cha Ukristo ambacho mara nyingi hakipo Yakobo 1:26.
“Kupitia msaada ambao Kristo anaweza kutoa, tutaweza kujifunza kudhibiti ulimi, vile vile alipojaribiwa kwa maneno ya haraka na ya hasira, hakufanya dhambi hata siku moja kwa midomo yake. Kwa utulivu wa subira alikutana na dhihaka, na dhihaka za wafanyakazi wenzake kwenye benchi ya seremala. Badala ya kujibu kwa hasira , angeanza kuimba mojawapo ya zaburi nzuri za Daudi; na marafiki zake kabla ya kutambua walichokuwa wakifanya, wangeungana naye katika wimbo huo. Mageuzi gani yangefanywa katika ulimwengu huu ikiwa wanaume na wanawake leo wangefuata mfano wa kristo katika matumizi ya maneno. —The SDA Bible Commentary [E. G. White Comments], vol. 7, p. 936.
b. Ni kwa Jinsi gani dini ya kweli na safi isiyo na ubinafsi inatenda kazi bila kujua? Yakobo 1:27.
“Kuwa mchapakazi, Kudumu kutenda kwa subira ambako huhitaji kujikana nafsi, ni kazi tukufu, ambayo mbingu huifurahia. Kazi ya uaminifu inakubaliwa na Mungu kuliko ibada yenye bidii zaidi na inayodhaniwa kuwa takatifu zaidi. Ni kufanya kazi pamoja na Kristo ndiyo ibada ya kweli. Maombi, maonyo, na maneno ya mdomoni ni matunda ya bei ndogo sana, ambayo mara nyingi huambatanishwa na kazi; lakini matunda ambayo hudhihirishwa kwa kutenda matendo mema, katika kuwajali wahitaji, yatima, na wajane, ni matunda yaliyo ya kweli/dhati, na kwa kawaida huota kwenye mti mzuri.”—Testimonies for the Church, vol. 2, p. 24.
Ijumaa
Oktoba 25
MASWALI TAFAKARI BINAFSI
1. Kwa nini tunaweza kuamini maisha yetu katika Mungu wa milele wa Mbinguni?
2. Ni nini wajibu wa wote ambao wamejikuta wakishindwa kujizuia?
3. Kwa nini ni muhimu kwangu kujisomea Neno la Mungu?
4. Elezea uhuru wa kweli ni nini.
5. Ninawezaje kusitawisha kiwango kikubwa zaidi cha dini ya kweli kutoka moyoni?