Back to top

Sabbath Bible Lessons

Masomo katika Waraka wa Yakobo

 <<    >> 
  SABATO, OKTOBA 5, 2024

Sadaka za sabato ya kwanza kwa ajili ya kanisa dogo lililoko Marekani; Reading, Pennsylvania, U.S.A.

Field ya Mashariki mwa Marekani (EUSF) imegawanyika katika maeneo Pennsylvania8081Allentown78 nane ya kijiografia yanayojumuisha majimbo Pennsylvania, New York, Reading, Connecticut, Rhode Island, Massachusetts, Maine, Vermont, Harrisburg, New hampshire. Katika kazi Pennsylvania kwa sasa inakua kwa haraka.

Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu 53% katika Baltimore jimbo hili ni watu wa kidini wanaojumuisha Wamethodisti, Walutheri, Wabaptisti, Wapentekost, na wengineo, wakiwa na wakatoliki28.3%

Katika siku za awali za ukoloni, Pennsylvania ilikuwa mahali pa kukimbilia kwa wahamiaji wanaotafuta uhuru wa kidini ili kuepuka mateso huko Ulaya. Historia hii bado inaonekana katika idadi kubwa ya waumini wa Jadi wa Amish ambao wanaendelea kukaa katika shamba kubwa katika jamii yote ya kata ya Lancaster, wakiwa wamevalia mavazi ya kawaida na kusafiri kwa farasi na gari la kubebea watu.

Kwa miaka mingi, washiriki wachache wa SDARM wameishi Pennsylvania na mafunzo ya umisionari yalitolewa hapa pia. Lakini uamsho wa sasa wa kupendezwa na ukweli uliopo ulianza mwaka wa 2016 katika jiji la Reading baada ya washiriki wawili kuhamia hapa kutoka New York. Kikundi kilipanuka na kuanza kukutana kila sabato alasiri, kikikusanyika katika bustani wakati wa kiangazi na kwenye nyumba ya dada wakati wa majira ya baridi kali. Baada ya miezi kadhaa ya kujifunza, wengi walibatizwa katika imani ya matengenezo.

Reading kuna idadi ya watu 95,000 na ni kituo cha kutengeneza vifaa vya umeme, vifaa vya matibabu, teknologia ya kuhifadhi nishati na zaidi. Kanisa letu hapa sasa ndio kubwa zaidi katika jimbo la Mashariki mwa Marekani.. Nafsi mpya zaidi zinatayarishwa kujiunga na watu wa mungu. Kwa sasa, tunaabudu katika kituo cha kukodi na tungependa kuthibitisha uwepo wetu kwa ajili ya kukua kwa kuwafikia walio nje zaidi. “popote pale kundi la waumini linapoinuliwa, nyumba ya ibada ijengwe….

”Katika sehemu nyingi ambapo ujumbe umehubiriwa na nafsi zimehubiriwa wamekubali, wako katika mazingira machache, na wanaweza kufanya kidogo tu kupata manufaa ambayo yangeipa kazi tabia. Mara nyingi hii inafanya kuwa ngumu kupanua kazi.”—Evangelism, p. 376.

Kwa hivyo, tunawasihi ndugu zetu na washirika kutoka duniani kote ili kutusaidia kuendeleza nyumba ya ibada katika eneo la Reading, ili roho nyingi zaidi ziweze kuletwa zizini. Ukarimu wako mzuri utathaminiwa sana, na Bwana atakubariki nawe.

Ndugu zenu kutoka Field ya Marekani Mashariki

 <<    >>