Jumapili
Oktoba 6
1. KUOMBA KWA HEKIMA
a. Kwa nini tunahitaji zaidi hekima ya kibinadamu maishani, na tunaweza kuipata kwa jinsi gani? Yakobo1:5.
“Tunahitaji kuwa na ujasiri mdogo sana katika kile ambacho mwanadamu anaweza kufanya na kujiamini zaidi katika kile ambacho mungu anaweza kufanya kwa kila nafsi inayoamini. Anatamani ili mpate kumfuata kwa imani. Anatamani sana wewe utazamie mambo makubwa kutoka kwake. —Christ’s Object Lessons, p. 146.
“Kusikia tu mahubiri ya sabato baada ya sabato, kusoma Biblia san, maelezo yake mstari kwa mstari, hautatufaidisha sisi au wale wanaotusikia, isipokuwa tukileta kweli za Biblia katika uzoefu wetu binafsi. Ufahamu, nia, mapenzi, lazima yakabidhiwe kwa udhibiti wa neno la Mungu. Kisha kupitia kazi ya Roho Mtakatifu maagizo ya neno yatakuwa kanuni za maisha.
“Unapomwomba Bwana akusaidie, mheshimu Mwokozi wako kwa kuamini ili upate baraka zake. Nguvu zote, hekima zote, ziko chini ya amri yetu. Tunapaswa kuomba tu.”—The Ministry of Healing, p. 514.
Jumatatu
Oktoba 7
2. KUIMARISHWA KWA IMANI
a. Tutafaidikaje ikiwa tunaiona hekima ya Mungu kuwa bora zaidi kuliko yetu, hata katika mambo ya kawaida ya maisha? Mithali 3:3–8.
“ ‘Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, Awapaye wote kwa ukarimu, wala Hakemei; naye Atapewa.’ Ahadi kama hiyo ni ya thamani kuliko shaba au dhahabu. kama kwa unyenyekevu wa moyo tutatafuta uongozi wa Mungu katika kila tatizo na mashaka, Neno Lake lakiri kwa ahadi kwamba utapokea jawabu la neema. Na Neno Lake haliwezi shindwa. Mbingu na nchi zitapita lakini Neno Lake halitapita. Mwamini Mungu na kamwe hautashindwa wala kuaibika. „Ni vema kumtumainia Mungu kuliko kuwatumainia wanadamu. Ni heri kumkimbilia Bwana, kuliko kuwatumainia wakuu”
“Haijalisha nafasi yoyote ya maisha au nyadhifa yoyote tutakayokuwa nayo, ama shughuli yoyote tutakayofanya, tunapaswa kuwa wanyenyekevu vya kutosha kutambua kuhitaji kwetu msaada, tunapaswa daima kuegemea kabisa katika mafundisho ya Mungu, tukitambua na kukiri majaliwa utoaji/Yake Wake wa kila kitu na kuwa waaminifu kumimina roho zetu kwa maombi. Zitegemee akili zako mwenyewe ndugu mpendwa, unapotembea katika maisha ya ulimwengu huu, nawe utavuna huzuni na kukatishwa tamaa. Mtegemee Mungu kwa moyo wako wote, naye ataongoza hatua zao katika hekma, na maslahi yako yatakuwa salama katika ulimwengu huu na ule ujao. Unahitaji nuru na maarifa. Waweza kuchukua mashauri ya Mungu ama ya moyo wako; waweza kutembea katika cheche za moto uliouwasha wewe mwenyewe ama utatembea katika nuru ya Bwana kutoka kwa Jua la Haki. ”—Testimonies for the Church, vol. 5, p. 427.
b. Kwa nini tunahitaji kujiondoa wenyewe kutoka kwa kutegemea sana watu wengine kwa mwongozo? Yeremia17:5–8.
“Mashaka yanapotokea, na matatizo yanapokukabili, usitafute msaada kwa wanadamu. Mtumainie yote kwa Mungu. Kitendo cha kuwaambia wengine magumu yetu hutufanya tu kuwa dhaifu, na haileti nguvu kwao. Inaweka juu yao mzigo wa udhaifu wetu wa kiroho, ambao hawewezi kuutatua. Tunatafuta nguvu za mwanadamu mpotovu, mwenye kikomo, wakati tunaweza kuwa na nguvu za Mungu asiyekosea, asiye na kikomo. ”—Christ’s Object Lessons, p. 146.
Jumanne
Oktoba 8
3. KUKUZA UIMARA ZAIDI
a. Ni sharti gani tunapaswa kutimiza kabla ya Bwana kujibu maombi yetu? Yakobo 1:6 (sehemu ya kwanza); Marko 11:24. Elezea mfano mmoja wa jinsi tunavyoweza kuamua kusitawisha nguvu katika jambo hili. 1 Wakorintho 6:3–5.
“Lakini ni wachache wanaotambua majukumu yaliyo juu ya watumishi wachache wanaobeba mizigo katika kazi hii. Ndugu huwaita mara kwa mara watu hawa kutoka kazini ili kushughulikia maswala yao madogo-madogo, au kusuluhisha kesi ya kanisa, ambavyo wanaweza na wanapaswa kushughulikia wenyewe.”Ikiwa mmoja wenu hukosa hekima, na aombe kwa Mungu, ambaye huwapa wote kwa ukarimu, na hakemei; naye atapewa. Lakini na aombe kwa imani, hakuna anayetetereka.”Lazima awe na bidii na mwenye mstahimilivu. Ikiwa hana msimamo, mwenye mashaka daima ikiwa Bwana atafanya kama alivyoahidi, hatapokea chochote.
“Wengi hutazamia wahudumu wao kuwaletea nuru kutoka kwa Mungu, wakionekana kufikiria hii ni njia rahisi kuliko kujipa shida ya kwenda kwa Mungu moja kwa moja kwa ajili yao wenyewe. Hao hupoteza sana. Ikiwa wangemfuata kila siku Kristo na kumfanya kuwa kiongozi na mshauri wao, wangeweza kupata ufahamu bora wa mapenzi Yake, na hivyo kupata uzoefu wa thamani. Kwa kukosa uzoefu huu, ndugu hawa wanaokiri kweli wanaota mioto ya wengine; hawamjui Roho wa Mungu na hawana ujuzi wa Mapenzi yake, na kwa hivyo huhamishwa kwa urahisi kutoka kwa imani yao. Hawana msimamo, kwa sababu waliamini wengine kupata uzoefu kwa niaba yao.”—Testimonies for the Church, vol. 2, pp. 643, 644.
b. Mtu anayedai kuwa Mkristo analinganishwa na nini ambaye imani yake huanza kuyumba? Yakobo 1:6 (sehemu ya mwisho); Mwanzo 49:4 (sehemu ya kwanza). Tunawezaje kuepuka hii?
“Imani ya Wakristo wengi itayumba ikiwa watapuuza kila mara kukutana pamoja kwa mkutano na sala.”—Ibid., vol. 4, p. 106.
“Chukua neno la kristo kama Uthibitisho wako. Je! Hajawaalika mje kwake? msiruhusu kamwe kuzungumza kwa njia isiyo na tumaini, kwa namna ya kukata tamaa. Kama mkifanya hivyo mtapoteza sana tumaini. Kwa kuangalia mwonekano na kulalamika matatizo na magumu yanapowapata, mnatoa uthibitisho wa imani iliyo dhaifu. Zungumza na kutenda kana kwamba imani yako haiwezi kushindwa.”— Christ’s Object Lessons, pp. 146, 147.
Jumatano
Oktoba 9
4. KUEPUKA MOYO ULIOGAWANYIKA
a. Tunawezaje kuhakikisha kwamba sala yetu ya kupata hekima itajibiwa? Luka 18:1; Yakobo1:6,7.
“Hili hitaji la hekima isiwe ombi lisilo na maana, likapotea akilini mara tu limalizikapo. Ni ombi ambalo huonesha hitaji madhubuti la ndani ya moyo, linaloibuka kutoka utambuzi wa kupungukiwa hekima kupambanua mapenzi ya mungu.
“Baada ya kufanywa ombi, kama jibu halijapatikana haraka, usichoke kusubiri na kutokuwa imara. Usitie shaka, shikilia ahadi, “Mwaminifu ni Yule akuitaye wewe, Yeye ambaye pia atafanya hivyo.” Kama mjane asiyekata tamaa, himiza hitaji lako, kuwa kidete katika lengo lako. Je, ni kitu muhimu na cha matokeo makubwa kwako? Hakika ndivyo. Basi usitie shaka, kwa Imani yako kuweza kujaribiwa. Kama jambo unalohitji ni la thamani, inastahili ukakamavu na bidii ya kazi. Unayo ahadi, kesha na omba. Kuwa imara na ombi litajibiwa; Je si Mungu aliyeahidi? Kama Ikikugharimu kitu kukipataa utakithamini zaidi ukipatapo. Umeambiwa wazi kwamba ukitia shaka uhitaji kufikiri kwamba utapata kitu chochote toka kwa Bwana. Angalizo limetolewa hapa ili usijechoka, bali kubaki imara juu ya ahadi. Kama ukiomba, atakupatia kwa ukarimu na hakemei.
“Hapa ndipo wengi hufanya kosa. Wanashaka katika lengo lao, na Imani yao hushindwa. Hii ndiyo sababu hawapokei kitutoka kwa BWANA, ambaye ni Chanzo cha nguvu zetu. Hakuna anayehitaji kwenda gizani, akijikwaa kama kipofu; maana BWANA ametoa nuru kama wataikubali katika namna aitoavyo, nasiyo kuchagua njia zao wenyewe. Anataka bidii katika kufanya wajibu wa kila siku. ”—Testimonies for the Church, vol. 2, pp. 130, 131.
b. Kwa nini tuepuke kuwa na nia mbili? Yakobo 1:8; Zaburi 86:11.
“Huku wakidai kuwa Wakristo, wengi wana umbo la ulimwengu juu yao, na mapenzi yao hayakuwekwa kwa Mungu. Wao ni wenye nia mbili, wakijaribu kumtumikia Mungu na mali kwa wakati mmoja….kwa kujaribu kuwatumikia mabwana wawili, hawana msimamo katika njia zao zote, na hawawezi kutegemewa….
“Kuna faida gani kusema mambo ya kupendeza, kudharau kazi ya shetani, na wakati huo huo kuingia katika utimilifu wa hila zake zote? Huku ni kuwa na nia mbili. ”—The SDA Bible Commentary [E. G. White Comments], vol. 7, p. 938.
Alhamisi
Oktoba 10
5. KUMKUMBUKA YAKOBO
a. Yesu anatoaje kielelezo jinsi tunavyopaswa kutoa maombi yetu kwa bidii ili tupate nguvu za kutimiza mapenzi ya Mungu? Mathayo 11:12.
“ ‘Ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.’ nguvu hii huchukua moyo wote. Kuwa na nia mbili ni kutokuwa na msimamo. Azimio, kujinyima na jitihada za kujitolea zinahitajika kwa ajili ya kazi ya maandalizi. Ufahamu na dhamiri viwe na umoja; lakini kama nia haijawekwa kufanya kazi, tutashindwa. Kila uwezo wa akili na hisia lazima zihusishwe. Ibada na maombi ya dhati lazima yachukue nafasi ya udhaifu. Ni kwa bidii tu, juhudi iliyodhamiriwa na imani katika wema wa kristo tunaweza kushinda, na kupata ufalme wa mbinguni. Muda wetu wa kufanya kazi ni mfupi. Kristo atakuja mara ya pili. ”—The SDA Bible Commentary [E. G. White Comments], vol. 1, p. 1096.
“Kwa ukweli mkuu ambao tumebahatika kuupokea, tunapaswa, chini ya nguvu za Roho Mtakatifu tungeweza kuwa njia hai za mwanga. Basi tungeweza kukikaribia kiti cha rehema; na kuona upinde wa ahadi, kupiga magoti kwa mioyo iliyopondeka, na kuutafuta ufalme wa mbinguni kwa nguvu ya kiroho ambayo ingeleta thawabu yake yenyewe. Tungeichukua kwa nguvu, kama alivyofanya Yakobo. Ndipo ujumbe wetu ungekuwa uweza wa Mungu uletao wokovu. Dua zetu zingejaa bidii, zilizojaa hisia ya hitaji letu kuu; na tusingekataliwa. Ukweli ungeonyeshwa kwa maisha na tabia, na kwa midomo iliyoguswa na makaa ya moto kutoka kwa madhabahu ya mungu.
“Wakati uzoefu huu ni wetu, tutainuliwa kutoka katika nafsi zetu maskini, za bei nafuu ambazo tumezipenda kwa upole. Tutatua mioyoni mwetu uwezo unaoharibika wa ubinafsi, na tutajawa na sifa na shukrani kwa Mungu. Tutamtukuza Bwana, Mungu wa neema yote, ambaye amemtukuza Kristo. Naye atadhihirisha uweza wake kupitia kwetu, akitufanya kuwa kama mundu wenye makali katika shamba la mavuno. Mungu anawaita watu wake wamdhihirishe. ”— Reflecting Christ, p. 217.
Ijumaa
Oktoba 11
MASWALI TAFAKARI BINAFSI
1. Elezea baadhi ya funguo muhimu za kupata hekima kuu kutoka Mbinguni.
2. Inakuwaje tunaporidhika na kutegemea maarifa ya kibinadamu?
3. Nifanyeje sehemu yangu kuwaweka huru watumishi ili kuzingatia roho mpya?
4. Ni katika sehemu gani za maisha ninaweza kuwa na nia mbili zaidi kuliko ninavyotambua?
5. Elezea nguvu na umuhimu wa mapambano ya Yakobo kwa siku za mwisho.